SERIKALI YASEMA KUNA HAJA YA KUANZISHA VITUO VYA KUENDELEZA TAALUMA YA TIBA MBADALA KATIKA KILA NGAZI YA UTAWALA | MALUNDE 1 BLOG

Thursday, December 17, 2020

SERIKALI YASEMA KUNA HAJA YA KUANZISHA VITUO VYA KUENDELEZA TAALUMA YA TIBA MBADALA KATIKA KILA NGAZI YA UTAWALA

  Malunde       Thursday, December 17, 2020


Mkurugenzi wa Sera na Mipango Wizara ya Afya Maendeleo ya jamii Jinsia ,Wazee na Watoto Bwana Edward Mbanga amesema kuwa kuna haja ya  kuanzisha vituo vya kuendeleza taaluma ya Tiba Asili na Tiba mbadala katika kila ngazi ya utawala wa serikali.

Mbanga amebainisha hayo  Disemba 16,2020 jijini Dodoma  wakati akifungua kikao kazi cha kuimarisha Huduma za Tiba Asili nchini.

Amesema bado kuna changamoto ya watu kushindwa kuthamini vyakao hasa katika matumizi ya tiba ya Asili kwani wengi hudhani ya kuwa vinavyotoka nje ya nchi huwa ni  bora zaidi kuliko vyakao .

 Mkurugenzi wa huduma za Tiba  Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii ,jinsia,Wazee na Watoto, Dkt Grace Maghebe amesema  lengo la kukutana kwao ni kutaka kuona tiba asili na tiba mbadala inawekwa kwenye utaratibu ambao utakuwa ni endelevu na pia kuinyanyua ionekane kama ni tiba sahihi kwa magonjwa kama ilivyo tiba nyingine yeyote.

Akizungumza kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Serikali,Mkurugenzi wa Uhakiki Ubora Dkt Eliud Eliakim amesema kama nchi wameamua kuendeleza tiba asili ili iweze kuwasaidia.

Katika  nchi ya Tanzania tiba asili ilianza kutambuliwa tangu mwaka 1960 ambapo kwa mara ya kwanza ilikuwa katika Wizara ya Utamaduni na Michezo na baada ya serikali kutambua kuwa hiyo ni tiba ya binadamu  mwaka 1990 walihamishia Wizara ya Afya.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post