SIMBA YATINGA HATUA YA PILI, SASA USO KWA USO NA FC PLATINUM LIGI MABINGWA

Licha ya kutoka suluhu ya bila kufungana katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Plateau United ya Nigeria, klabu ya Simba imefanikiwa kusonga mbele katika michuano hiyo kwa ushindi jumla wa goli 1-0 walioupata katika mchezo wa awali wa ugenini uliochezwa wiki iliyopita kwenye uwanja wa New Jos.

Katika mchezo huo wa awali goli pekee la Simba lilifungwa na kiungo Mzambia, Clatous Chama akimaliza kazi nzuri iliyofanywa na Winga Luis Miquissone.

Sasa mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) watakutana na FC Platinum ya Zimbabwe ambayo imetinga hatua hiyo baada ya kuwafunga Costa do Sol ya Msumbiji kwa ushindi wa jumla ya goli 4-1 baada ya kushinda 2-1 na kisha kushinda goli 2-0 katika mchezo wa marudianoa uliochezwa leo kwenye mji wa Bulawayo.

Katika mchezo huo, Simba itaanzia ugenini katika mchezo utakaochewa kati ya Desemba 22 au 23 katika uwanja wa National Sport na kisha watarudiana kati ya Januari 5 au sita katika uwanja wa Mkapa.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post