SHIRIKA LA AGRI THAMANI LATOA MAFUNZO YA LISHE BORA KWA WAJUMBE 312 WA SERIKALI ZA MITAA MANISPAA YA BUKOBA

 

MBUNGE wa Viti Maalumu Tanzania Bara kupitia (NGOs)  Neema Lugangira (Mb) ambaye pia ni Mkugenzi wa Shirika Agri Thamani akitoa mafunzo kwa wenyeviti na wajumbe wa Viti Maalumu wa Serikali Mitaa Manispaa ya Bukoba

MBUNGE wa Viti Maalumu Tanzania Bara kupitia (NGOs)  Neema Lugangira (Mb) ambaye pia ni Mkugenzi wa Shirika la Agri Thamani akitoa mafunzo kwa wenyeviti na wajumbe wa Viti Maalumu wa Serikali Mitaa Manispaa ya Bukoba
AFISA Elimu ya Watu Wazima Manispaa ya Bukoba akiishukuru Shirika la Agri Thamani  kutoa Mafunzo ya kutengeneza sabuni ya Maji kwa Walimu wa Afya wa Shule zote Manispaa ya Bukoba na Wanawake wa Manispaa hiyo
MBUNGE wa Viti Maalumu Tanzania Bara kupitia (NGOs)  Neema Lugangira (Mb) ambaye pia ni Mkugenzi wa Shirika la Agri Thamani kushoto akishauriana jambo na waratibu wa miundombinu ya mafunzo hayo
MBUNGE wa Viti Maalumu Tanzania Bara kupitia (NGOs)  Neema Lugangira (Mb) ambaye pia ni Mkugenzi wa Shirika Agri Thamani kushoto akiwa na Mratibu wa Agri Thamani Kagera
Viongozi wa Serikali za mitaa wakifuatilia mafunzo hayo
Viongozi wa Serikali za mitaa wakifuatilia mafunzo hayo

MBUNGE wa Viti Maalumu Tanzania Bara kupitia (NGOs)  Neema Lugangira (Mb) ambaye pia ni Mkugenzi wa Shirika la Agri Thamani wametoa mafunzo ya lishe bora kwa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa na Wajumbe wake kutoka Mitaa yote 66 ya Bukoba Manispaa mkoani Kagera.

Mafunzo haya yameandaliwa kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba yakiwa na lengo kuhimiza suala la lishe bora kwenye  maeneo yao.

Shirika la Agri Thamani limeamua kutoa mafunzo haya ikiwa ni jitihada ya kuhakikisha kuwa Viongozi hawa wanachangia ipasavyo katika Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya 2020-2025 ya Chama Tawala, Chama Cha Mapinduzi (CCM) 

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo Mhe Neema Lugangira amesema kwamba kwa awamu ya kwanza Mafunzo hata yatatolewa kwenye Serikali za Mitaa za Wilaya zitakazochaguliwa kutoka Mikoa mbalimbali nchini. 

Mafunzo hayo yamewanufaisha viongozi 312 na kupitia Ushiriki wao kama Viongozi kuanzia Ngazi ya Jamii huku akieleza  Agri Thamani ina amini kama Taifa tutaweza kufikia lengo la kuimarisha lishe bora nchini kama ilivyoainishwa kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments