RAIS MAGUFULI ASAMEHE WAFUNGWA 3316...AGOMA KUNYONGA 256


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli amewapunguzia adhabu wafungwa   256 waliohukumiwa kunyongwa ambapo amesema sasa wapewe kifungo cha maisha.

Rais Magufuli ametoa msamaha huo leo Disemba 9,2020 ikiwa ni siku ya kuadhimisha miaka 59 ya Uhuru wa Tanganyika wakati akiwaapisha Mawaziri na Manaibu Waziri aliowateua Disemba 5,2020. 

"Kati ya hawa 256 wapo waliohukumiwa kunyongwa kwa sababu ya kuua.  Nimeshindwa kuwaua naomba mnisamehe kwa hilo",amesema Rais Magufuli. 

"Pia Wafungwa 3316 wa makosa mbalimbali wapunguziwe adhabu na wengine kusamehewa",ameongeza

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post