POLISI WACHUNGUZA TUKIO LA MWANAMKE KUJIFUNGUA KUKU | MALUNDE 1 BLOG

Monday, December 7, 2020

POLISI WACHUNGUZA TUKIO LA MWANAMKE KUJIFUNGUA KUKU

  Malunde       Monday, December 7, 2020

Kushoto ni Kamanda wa polisi mkoa wa Kigoma, James Manyama na kulia ni Kuku aliyekutwa kwenye kizazi.

Jeshi la polisi mkoa wa Kigoma limesema kuwa kuku aliyekutwa kwenye kizazi cha mwanamke mkoani humo, atapelekwa kwenye Maabara ya Mkemia wa Serikali kwa ajili ya kuchunguzwa kwani si kawaida kwa binadamu kujifungua kiumbe cha namna ile.

Kauli hiyo imetolewa na Kamanda wa polisi mkoa wa Kigoma James Manyama, wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani humo, na kusema kuwa tukio la mwanamke huyo kujifungua kuku lilitokea siku ya Desemba 5, 2020, katika kituo cha afya Uvinza.

"Kwa kuwa tukio hili siyo la kawaida kwenye jamii, jeshi la polisi tutachukua kiumbe hicho kwa ajili ya kupeleka Maabara ya Mkemia wa Serikali kwa ajili ya uchunguzi zaidi kwani siyo kawaida kwa binadamu kujifungua kuku", amesema Kamanda Manyama.

Chanzo- EATV

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post