NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE, MHE. OLE NASHA ALIVYOPOKELEWA WIZARANI


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. William Tate Ole Nasha ameahidi ushirikiano kwa Watumishi wa Wizara katika kuhakikisha Wizara inakuwa na matokeo chanya yenye tija kwa jamii na Taifa kwa ujumla katika utekelezaji wa majukumu yake.

Mhe. Ole Nasha ameyasema hayo aliwapowasili Wizarani mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli katika hafla iliyofanyika Ikulu, Chamwino jijini Dodoma tarehe 9 Desemba 2020.

Mhe. Ole Nasha ambaye alipokelewa na Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki amesema kuwa yupo tayari kujifunza kutoka kwa Watumishi wote ili kuiwezesha Wizara kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Kwa upande wake. Prof. Kabudi alimhakikishia Mhe. Ole Nasha ushirikiano wake binafsi na kutoka kwa Watumishi wote na kwamba uwepo wake utaongeza nguvu za kuifikisha Wizara katika viwango vya juu kiutendaji.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post