HUNGARY NA TANZANIA ZATILIANA SAHIHI UFADHILI WA WANAFUNZI WA KITANZANIA


Tanzania na Hungary zimetiliana saini makubaliano ya ufadhili kwa Wanafunzi zaidi ya 30 wa Kitanzania kwenda kusoma katika vyuo vikuu vya Nchini Hungary katika kipindi cha miaka mitatu kuanzia 2021 hadi 2023.

Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Nchini Ujerumani anayeiwakilisha pia Hungury Dkt. Abdalla Possi amesema makubaliano hayo yanatoa fursa kwa Wanafunzi wa Tanzania kupata elimu katika Vyuo vya Hungary kwa masomo ya shahada ya kwanza,shahada ya Uzamili na shahada ya uzamivu katika maeneo mbalimbali ya kitaaluma.

Ameongeza kuwa makubaliano hayo ni kielelezo kingine cha uhusiano mzuri uliopo baina ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Hungury na kwamba nafasi hizo zitaendelea kuongezeka kutokana na Serikali ya Hungary kufurahishwa na muitikio wa Watanzania wanaoomba nafasi hizo za masomo.

Katika tukio jingine Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Ujerumani umefungua rasmi ofisi ya muwakilishi wa heshima wa Tanzania iliyoko katika mji wa Bruno katika nchi ya Jamhuri ya Czech.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imemuidhnisha Bw. Roman Grolig kuwa mwakilishi wa heshima wa Tanzania katika Jamhuri ya Czech ambapo mji wa Bruno ni mji wa kimkakati ambapo kila mwaka mamlaka za mji huo huandaa miongoni mwa mambo mengine maonesho makubwa ya biashara na utaliibarani Ulaya.

Mji wa Bruno pia ni makao makuu ya Baraza la biashara la Czech – Tanzania.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments