MWILI WA MTANGAZAJI WA REDIO MOSHI FM DEOGRATIUS KESSY WAZIKWA KIJIJINI KWAO URU NJARI

Mazishi ya Mwili wa Mwandishi wa habari na Mtangazaji wa redio Moshi FM, Deogratius Kessy yakiendelea leo Jumatano Desemba 16,2020 kijijini kwao Uru Njari Moshi Vijijini.
Mwandishi wa habari na Mtangazaji wa redio Moshi FM, Deogratius Kessy enzi za uhai wake
Mwandishi wa habari na Mtangazaji wa redio Moshi FM, Deogratius Kessy enzi za uhai wake.  

Na Mwandishi wa Malunde 1 blog - Moshi
Mwili wa Mwandishi wa habari na Mtangazaji wa redio Moshi FM, Deogratius Kessy (26) aliyefariki dunia katika ajali baada ya gari alilokuwa amepanda kuacha njia na kugonga bajaji umezikwa kijijini kwao Uru Njari Moshi Vijijini Mkoani Kilimanjaro katika makaburi ya familia leo Jumatano Desemba 16,2020.

Meneja vipindi wa redio Moshi Fm, Rodrick Makundi amesema watamkumbuka daima Deogratius Kessy kwa mambo mengi mazuri kwani alikuwa mchapakazi mzuri. 

"Tumepoteza mtu muhimu sana. Deogratius alikuwa akitangaza kipindi cha burudani cha The base show. Alikuwa anatoa ushauri pale unapohitajika pia tulijifunza mambo mengi mazuri kutoka kwake kutokana na ubunifu wake kwenye vipindi alivyokuwa akifanya",amesema Makundi. 

Kamanda wa polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Emmanuel Lukula alisema ajali hiyo imetokea Ijumaa Desemba 11,2020 saa 2 usiku katika barabara ya Getifonga eneo la kona ya kibao cha kuelekea Kahe.

Alisema gari aina ya Noah lililokuwa limepakia watu zaidi ya wawili likitokea Newland kwenda mjini Moshi ilipofika katika kona hiyo liligonga bajaji na kuwajeruhi watu watatu na mwandishi huyo kufariki dunia wakati akipatiwa matibabu hospitali ya rufaa Mkoa wa Kilimanjaro.

“Kwenye ile Noah watu wawili walipata zaidi majeraha na waliwahishwa hospitali ila mmoja ndiyo amefariki. Kwenye ile bajaji mama mmoja alivunjika miguu yote miwili na majeruhi wote wanaendelea na matibabu,” amesema.

Kifo cha mwandishi huyo kimetokea ikiwa zimepita siku 35 tangu mwandishi mwingine wa habari wa redio Kili FM mjini Moshi, Benedick Kuzwa kufariki dunia katika ajali.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post