Picha : MAONESHO YA BIASHARA NA TEKNOLOJIA YA MADINI YAWA KIVUTIO SHINYANGA...SASA MNARA KUJENGWA OLD SHINYANGA

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kulia) akimpokea Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini Tanzania Prof. Idris Kakula katika viwanja vya Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga katika eneo la Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga ili kufunga maonesho hayo leo Jumanne Desemba 1,2020. 

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini Tanzania Prof. Idris Kakula amefunga Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga katika eneo la Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.

Prof. Kakula amefunga Maonesho hayo ya Biashara na Teknolojia ya Madini yaliyoongozwa na kauli mbiu ya ‘Biashara na madini ni chachu ya maendeleo Shinyanga’ leo Jumanne Desemba 1,2020. 

Prof. Kakula ameupongeza uongozi wa serikali ya Mkoa wa Shinyanga ukiongozwa na Mkuu wa Mkuu wa mkoa Zainab Telack pamoja na wadau wote kwa kushiriki katika kuratibu na kufanikisha maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini ambayo ni chachu ya kufanya mabadiliko ya kuongeza teknolojia ili kuinua uchumi.

Aidha ametoa wito kwa wafanyabiashara kutoka nje ya nchi kuja nchini Tanzania ili kuuza madini yao huku akibainisha kuwa Serikali inaendelea kuboresha maisha ya wachimbaji wadogo na itaendelea kuimarisha masoko ya madini 

“Kwa dhati kabisa nitumie fursa hii kuwapongeza wafanyabiashara wanaoendelea kulipa kodi kwa hiari na kufanya kazi kwa kufuata sheria na wale wachache wanaotaka kupotoka tuwashauri kufanya biashara kwa njia ya halali”,ameongeza.

Prof. Kakula pia ameziomba Taasisi za Kibenki ziangalie namna ya kuwakopesha wachimbaji wadogo wa madini badala ya kuwatazama kuwa ni watu wasiokopesheka.

Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akimwakilisha Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack amesema Maonesho hayo yatakuwa chachu ya kuongeza ubunifu na kuongeza uchumi wa mtu mmoja mmoja.

 “Zaidi ya watu 3000 wametembelea eneo hili la maonesho katika viwanja tulivyovipa jina la Zainab Telack. Maonesho haya yametoa fursa kwa wananchi kuonesha biashara, teknolojia ya madini na kuuza vyakula. Eneo hili litakuwa eneo la kudumu kwa ajili ya maonesho mbalimbali”,amesema.

Amesema kutokana na mwitikio mkubwa wa wafanyabiashara na wadau mbalimbali kufika katika eneo la maonesho, wameongeza siku mbili zaidi kuendelea na maonesho ya biashara na teknolojia ya madini katika eneo hilo.

“Shinyanga ni yetu sote ni lazima tuijenge sote, sisi kama wana shinyanga tuna nafasi ya kuendeleza mkoa wetu. Shinyanga itajengwa na Wana Shinyanga na walio nje ya Shinyanga karibuni tuijenge shinyanga yetu”,amesema Mboneko.

Naye Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA) mkoa wa Shinyanga, Dk. Kulwa Ezekiel Meshack amesema maonesho katika eneo hilo la Maonesho la Butulwa Old Shinyanga patajengwa mnara wa kumbukumbu na sanamu ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wake katika sekta ya biashara na madini mkoani Shinyanga.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini Tanzania Prof. Idris Kakula akizungumza wakati akifunga Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga  katika eneo la Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga leo Jumanne Desemba 1,2020. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini Tanzania Prof. Idris Kakula akizungumza wakati akifunga Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga katika eneo la Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini Tanzania Prof. Idris Kakula akizungumza wakati akifunga Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga katika eneo la Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini Tanzania Prof. Idris Kakula akizungumza wakati akifunga Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga katika eneo la Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini Tanzania Prof. Idris Kakula akizungumza wakati akifunga Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga katika eneo la Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza wakati wa kufunga Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga katika eneo la Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza wakati wa kufunga Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga katika eneo la Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.
Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA) mkoa wa Shinyanga, Dk. Kulwa Ezekiel Meshack akizungumza wakati wa kufunga Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga katika eneo la Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.
Rais wa Shirikisho la Wachimbaji Wadogo Tanzania (FEMATA), John Bina akizungumza wakati wa kufunga Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga katika eneo la Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.
Meza kuu 
Burudani kutoka kundi la Ngoma za Asili la Wanzingiza likiendelea
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela akizungumza wakati wa kufunga Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga katika eneo la Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.
Kwaya ya AIC Shinyanga ikitoa burudani
Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini Tanzania Prof. Idris Kakula akitoa zawadi ya cheti kwa washiriki wa maonesho ya Biashara na Teknlojia ya Madini, kushoto ni mwakilishi wa Meneja wa Benki ya TPB , Bi. Lupiana 
Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini Tanzania Prof. Idris Kakula akitoa zawadi ya cheti kwa washiriki wa maonesho ya Biashara na Teknlojia ya Madini, kushoto ni Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo, Anwali Saidi.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini Tanzania Prof. Idris Kakula akiendelea kutoa zawadi ya vyeti kwa washiriki wa maonesho ya Biashara na Teknlojia ya Madini.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini Tanzania Prof. Idris Kakula akitoa zawadi ya cheti kwa washiriki wa maonesho ya Biashara na Teknlojia ya Madini, kushoto ni Mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Shinyanga Dk. Meshack Kulwa.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini Tanzania Prof. Idris Kakula akitoa zawadi ya cheti kwa washiriki wa maonesho ya Biashara na Teknlojia ya Madini, kushoto ni mwakilishi wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Twiga Minerals 'Buzwagi & Bulyanhulu'
Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini Tanzania Prof. Idris Kakula akitoa zawadi ya cheti kwa washiriki wa maonesho ya Biashara na Teknlojia ya Madini, kushoto ni Mkugenzi wa Kampuni ya Shinyanga Best Iron, Kashi Salula Gacha
Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini Tanzania Prof. Idris Kakula akitoa zawadi ya cheti kwa washiriki wa maonesho ya Biashara na Teknlojia ya Madini, kushoto ni mwakilishi wa Kampuni ya Canon ' Shujaa'
Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini Tanzania Prof. Idris Kakula akitoa zawadi ya vyeti kwa washiriki wa maonesho ya Biashara na Teknlojia ya Madini
Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini Tanzania Prof. Idris Kakula akitoa zawadi ya vyeti kwa washiriki wa maonesho ya Biashara na Teknlojia ya Madini
Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Shinyanga, Dk. Meshack akizungumza wakati wa zoezi la kugawa zawadi kwa washiriki wa maonesho.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini Tanzania Prof. Idris Kakula akitoa zawadi kwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Mhe. Jasinta Mboneko kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainab Telack kwa kufanikisha maonesho hayo.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini Tanzania Prof. Idris Kakula akitoa zawadi kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Geofrey Mwangulumbi kwa kufanikisha maonesho hayo.
Mwenyekiti wa Chama Cha Wachimbaji wadogo wa madini mkoa wa Shinyanga (SHIREMA) akizungumza
Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini Tanzania Prof. Idris Kakula akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Mhe. Jasinta Mboneko (kulia).
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kulia) akimuongoza Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini Tanzania Prof. Idris Kakula kutembelea mabanda ya wadau wa biashara na madini katika viwanja vya Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga katika eneo la Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.  
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko  na viongozi mbalimbali wakimuongoza Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini Tanzania Prof. Idris Kakula kutembelea mabanda ya wadau wa biashara na madini katika viwanja vya Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga katika eneo la Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.  
Kulia ni Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini Tanzania Prof. Idris Kakula akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Uuundaji wa Vifaa vya uchimbaji na uchenjuaji madini ya Shinyanga Best Iron, Kashi Salula Gacha katika viwanja vya Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga katika eneo la Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga. 
Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini Tanzania Prof. Idris Kakula akiwa katika Banda la Kampuni ya Vinywaji ya East African Spirits Ltd kwenye viwanja vya Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga katika eneo la Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.  
Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini Tanzania Prof. Idris Kakula akiwa katika banda la Kampuni ya Vinywaji ya Jambo Food Products katika viwanja vya Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga katika eneo la Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga. 
Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini Tanzania Prof. Idris Kakula akiwa katika banda la TANESCO katika viwanja vya Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga katika eneo la Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga. 
Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini Tanzania Prof. Idris Kakula akiwa katika banda la Kampuni ya Mawasiliano ya TTCL katika viwanja vya Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga katika eneo la Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga. 
Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini Tanzania Prof. Idris Kakula akiwa katika banda la Benki ya NMB katika viwanja vya Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga katika eneo la Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga. 
Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini Tanzania Prof. Idris Kakula akiwa katika banda la Benki ya CRDB katika viwanja vya Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga katika eneo la Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga. 
Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini Tanzania Prof. Idris Kakula akiwa katika banda la Benki ya CRDB katika viwanja vya Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga katika eneo la Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga. 
Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini Tanzania Prof. Idris Kakula akiwa katika banda la Benki ya TPB katika viwanja vya Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga katika eneo la Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga. 
Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini Tanzania Prof. Idris Kakula akiwa katika banda la Exim katika viwanja vya Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga katika eneo la Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga. 
Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini Tanzania Prof. Idris Kakula akiwa katika banda la Benki ya NBC  katika viwanja vya Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga katika eneo la Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga. 
Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini Tanzania Prof. Idris Kakula akiwa katika banda la NHIF katika viwanja vya Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga katika eneo la Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga. 
Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini Tanzania Prof. Idris Kakula akiwa katika banda la Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Dhahabu ya Twiga Minerals katika viwanja vya Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga katika eneo la Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga. 
Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini Tanzania Prof. Idris Kakula akiwa katika banda la Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Stamigold  katika viwanja vya Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga katika eneo la Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga. 
Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini Tanzania Prof. Idris Kakula akiwa katika banda Wachimbaji wadogo wa Madini wa mgodi wa Mwakitolyo katika viwanja vya Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga katika eneo la Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga. 
Hapa ni katika banda ya Tume ya Madini
Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini Tanzania Prof. Idris Kakula akiendelea kutembelea mabanda ya wadau
Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini Tanzania Prof. Idris Kakula akiendelea kutembelea mabanda ya wadau

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments