MADIWANI MANISPAA YA SHINYANGA WAAPISHWA RASMI, WAONYWA KUWA CHANZO CHA MIGOGORO


Madiwani wa Halmashauri ya manispaa ya Shinyanga wakiapa kiapo cha uadilifu na utiii

Na Marco Maduhu -Shinyanga. 
Madiwani wa Halmashauri ya manispaa ya Shinyanga, wameapishwa rasmi kuwa madiwani halali, mara baada ya kushinda kwenye uchaguzi mkuu ambao ulifanyika Oktoba 28 mwaka huu na kuonywa kutokuwa chanzo cha migogoro.


Zoezi la kuapishwa madiwani hao limefanyika leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo, na kuhudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini, lililoendeshwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkoa wa Shinyanga Mary Mrio. 

Akizungumza wakati wa kutoa Salamu, Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko amewataka madiwani hao wakafanya kazi kwa ushirikiano na watendaji wote wa Serikali, na wasiwe chanzo na kuibua migogoro bali wakawe watatuzi wa migogoro ndani ya jamii. 

“Nawaomba madiwani mkawe na ushirikiano na viongozi kwenye maeneo yenu, kwa ajili ya kujenga maendeleo ya manispaa ya Shinyanga na kuwatumikia wananchi na msiwe chanzo cha kuibua migogoro,”alisema Mboneko. 

“Pia mkasimamie miradi ya maendeleo, na mapato ya Serikali ili tupate fedha za kuwaletea maendeleo wananchi ikiwamo ujenzi wa vyumba vya madarasa, pamoja na kusimamia asilimia 10 za mikopo ya wanawake, vijana na walemavu, ili tuwainue kiuchumi wananchi wetu,”aliongeza. 

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira Patrobasi Katambi, amewataka madiwani hao wakafanye kazi kwa ajili ya maslahi ya wakazi wa Shinyanga na siyo kutanguliza maslahi binafsi, huku akiahidi kutoa ushirikiano kwao, pamoja na viongozi wote na kuomba wamtumie ili wapambane kuleta maendeleo Shinyanga. 

Naye Mstahiki Meya wa Manispaa ya Sinyanga David Nkulila, ameahidi ushirikiano na Madiwani pamoja na watumishi wa Serikali, kwa ajili ya Mstakabali wa maendeleo ya manispaa hiyo, sambamba na kutatua matatizo ya migogoro mbalimbali, ili mji wa Shinyanga uwe mahali salama pa kuishi. 

TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI
 
Naibu Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu kazi, vijana na ajira Patrobas Katambi, akitoa neno mara baada ya Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga kumaliza kuapishwa.
 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akitoa neno la Salamu mara baada ya Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga kumaliza kuapishwa.
Katibu Tawala wa wilaya ya Shinyanga Boniphace Chambi, akizungumza kwenye zoezi hilo la uapisho wa madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Mstahiki Meya wa manispaa ya Shinyanga David Nkulila, akizungumza mara baada ya kumaliza kuapishwa.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi, akizungumza kwenye zoezi hilo la kuapishwa madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
Mstahiki Meya wa manispaa ya Shinyanga David Nkulila, akiapishwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkoa wa Shinyanga Mary Mrio. 
Naibu Meya wa manispaa ya Shinyanga Ester Makune akiapishwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkoa wa Shinyanga Mary Mrio.
Diwani wa Kata ya Mjini Gulam Mkadamu, ambaye alikuwa Mstahiki Meya wa manispaa ya Shinyanga kipindi kilichopita akiapishwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkoa wa Shinyanga Mary Mrio.
Diwani wa Kata ya Chibe John Kisandu, ambaye alikuwa Naibu Meya wa manispaa ya Shinyanga , akiapishwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkoa wa Shinyanga Mary Mrio.
Zoezi la kuapisha madiwani likiendelea.
Zoezi la kuapisha madiwani likiendelea.
Zoezi la kuapisha madiwani likiendelea.
Zoezi la kuapisha madiwani likiendelea.
Zoezi la kuapisha madiwani likiendelea.
Zoezi la kuapisha madiwani likiendelea.
Zoezi la kuapisha madiwani likiendelea.
Zoezi la kuapisha madiwani likiendelea.
Zoezi la kuapisha madiwani likiendelea.
 

Zoezi la kuapisha madiwani likiendelea.
 

Zoezi la kuapisha madiwani likiendelea.
Zoezi la kuapisha madiwani likiendelea.
Zoezi la kuapisha madiwani likiendelea.
Madiwani wa Halmashauri ya manispaa ya Shinyanga wakiapa kiapo cha uadilifu na utii mara baada ya kumaliza kuapishwa kuwa Madiwani Rasmi.
Wananchi wa manispaa ya Shinyanga wakishuhudia uapisho wa madiwani wa Halmashauri hiyo.
Wananchi wakiendelea kushuhudia zoezi la uapisho wa madiwani wa Halmashauri ya manispaa ya Shinyanga.
Wananachi na viongozi mbalimbali wa Serikali wakishuhudia zoezi hilo la Uapisho wa Madiwani wa Halmashauri ya manispaa ya Shinyanga.
Viongozi wa Chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga mjini, akishuhudia zoezi la uapisho wa Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Zoezi la uapisho madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga likiendelea kushuhudiwa.
Zoezi la uapisho madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga likiendelea kushuhudiwa.
Zoezi la uapisho madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga likiendelea kushuhudiwa.
Zoezi la uapisho madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga likiendelea kushuhudiwa.
Pongezi zikitawala mara baada ya madiwani wa Halmashauri ya manispaa ya Shinyanga kumaliza kuapishwa.
Furaha zikitawala mara baada ya madiwani wa Halmashauri ya manispaa ya Shinyanga kumaliza kuapishwa.
Madiwani wa Halmashauri ya manispaa ya Shinyanga, wakiingia ukumbini kuendelea na Baraza mara baada ya kumaliza kuapishwa.
Madiwani wa Halmashauri ya manispaa ya Shinyanga, wakiingia ukumbini kuendelea na Baraza mara baada ya kumaliza kuapishwa.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga David Nkulila, wa kwanza, akielekea kwenye ukumbi kwa ajili ya kuanza Baraza la Madiwani mara baada ya kumaliza kuapishwa, katikati ni Naibu Waziri Ofisi ya Nchi ya Waziri mkuu kazi, vijana, na ajira, Patrobas Katambi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini, akifuatiwa na Naibu Meya Ester Makune.
Mstahiki Meya wa manispaa ya Shinyanga David Nkulila, wapili kutoka kushoto, akifungua Baraza la Madiwani.
Madiwani wa Halmashauri ya manispaa ya Shinyanga wakipiga picha ya pamoja na viongozi.

Na Marco Maduhu- Shinyanga.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments