ALIYEMKABA MESSI AFARIKI DUNIA


Beki wa Mamelodi Sundowns Motjeka Madisha (kushoto) akikabana na Lionel Messi.
Beki wa Mamelodi Sundowns Motjeka Madisha

Beki wa Mamelodi Sundowns Motjeka Madisha, amefariki dunia akiwa na miaka 25. Taarifa zimeeleza kuwa Madisha amefariki kwenye ajali ya gari alfajiri ya leo Desemba 13, 2020 huko Johannesburg Afrika Kusini.

Madisha ameichezea Mamelodi zaidi ya mechi 130 na kushinda makombe matatu ya ligi kuu pamoja na Ligi ya Mabingwa Afrika na Super Cup.

Beki huyo ni miongoni mwa wachezaji waliokuwa tegemeo kwenye mafanikio ya Mamelodi chini ya kocha Pitso Mosimane, ambapo mbali na ligi pamoja na klabu bingwa pia walishinda mataji mbalimbali kama Telkom Knockout, the Nedbank Cup.

Pia nyota huyo ameichezea timu ya taifa ya Afrika Kusini akijihakikishia nafasi kwa miaka ya hivi karibuni.

Motjeka Madisha pia alimkaba Lionel Messi kwenye mchezo wa kirafiki uliopigwa Mei 16, 2018 na kumalizika kwa Barcelona kushinda magoli 3-1.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post