AKAMATWA KWA KUDAIWA KUMUUA HAWARA YAKE , MTOTO WA HAWARA


Kamanda wa Polisi mkoani Kagera Revocatus Malimi.

Jeshi la Polisi mkoani Kagera linamshikilia mtu mmoja Festo Venance mwenye umri wa miaka 38 kwa tuhuma za kuwaua watu wawili na kumjeruhi mwingine mmoja, katika kijiji cha Kumzuza wilayani Ngara.

Kamanda wa Polisi mkoani Kagera Revocatus Malimi amewataja waliouawa kuwa ni Magreth Jacob mwenye umri wa miaka 33 ambaye alikuwa hawara wa mtuhumiwa, na mtoto mdogo Jonam Niyonzima mwenye umri wa miaka mitatu, huku aliyejeruhiwa akitajwa kuwa ni Penina Joseph Mwenye umri wa miaka 40, ambaye amelazwa katika hospitali ya Murgwanza wilayani humo.

Kamanda huyo amesema kuwa sababu ya mauaji hayo bado haijafahamika na mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa lakini bado hajakiri kuhusika na mauaji hayo, ingawa kuna baadhi ya mazingira yanaonyesha kuhusika kwake, ikiwamo nguo alizokuwa amevaa kukutwa na damu.

CHANZO - EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post