WAZIRI WA NISHATI AFANYA ZIARA MKOANI SHINYANGA, AONYA KATA KATA HOVYO YA UMEME

Waziri wa Nishati Dkr Medard Kalemani akizungumza na watumishi wa Shirika la umeme Tanzania TANESCO Mkoa wa Shinyanga.

Na Marco Maduhu  -Shinyanga. 
Waziri wa Nishati Dk. Medard Kalemani, amelionya Shirika la umeme Tanzania (TANESCO), kuacha tabia ya kukata kata umeme hovyo.

Kalemani ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Chato ,amebainisha hayo leo, wakati akizungumza na watumishi wa Shirika hilo mkoani Shinyanga, ambapo aliambatana na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Steven Byabato, Kaimu kamishina wa Nishati Edson Wingabo, Kaimu meneja Mwandamizi Rasilimali Watu kutoka TANESCO makao makuu Festo Mkolla, pamoja na Kaimu Meneja Mwandamizi wa TANESCO Kanda ya Magharibi Mhandisi John Kiduko 

Amesema kitendo cha kukata kata umeme hovyo tena bila taarifa hapendezwi nacho, na kubainisha tabia hiyo itakuja kumfukuzisha mtu kazi. 

"Naombeni sana Mameja wa TANESCO nchi nzima acheni tabia ya kukata kata umeme hovyo, tena wakati mwingine bila hata kutoa taarifa ,fanye kazi zenu kwa ufanisi, na eneo ambalo halina umeme mna hatarisha usalama", amesema Dk. Kalemani. 

Pia amewataka wafanyakazi hao waache kufanya kazi kimazoea, bali wabadilike na kufanya kazi kwa kasi, ubunifu, na kwa usahihi, ili kutoa huduma Stahiki ya usambazaji umeme kwa wananchi.

"Fanyeni kazi zenu kwa ufanisi kama mlivyofanya kwenye miaka mitano iliyopita mmefanya kazi vizuri sana, na hii ilitusaidia sisi wagombea wa CCM kwenye kipindi cha Kampeni katika uchaguzi mkuu uliopita, kunadi sera zetu kwa wananchi na hatimaye kupata ushindi wa kishindo kutokana na TANESCO kufanya kazi vizuri ya kusambaza Nishati ya umeme kwenye maeneo mengi," ameeleza Dk. Kalemani. 
 
Katika hatua nyingine, amewaonya watumishi hao kuacha kutoa lugha chafu kwa wateja, pamoja na kuacha kujihusisha kufanya kazi na vishoka, huku akitoa miezi mitatu ndani ya mkoa huo wananchi wote wawe wamesha sambaziwa huduma ya umeme. 

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Nishati Steven Byabato, alikazia suala la kubainisha wateja halali ambao wanatumia Nishati ya umeme wabainishwe hadi kufikia januari 31 mwakani, pamoja na kuwafichua wezi wa umeme na kuwachukulia hatua. 

Aidha Kaimu Meneja Mwandamizi Rasilimali watu kutoka Shirika la TANESCO Makao Makuu Festo Mkolla, amebainisha maagizo yote ambayo yametolewa na viongozi hao atayafanyia kazi ili kuongeza ufanisi wa utendaji kazi kwa watumishi wa Shirika hilo. 

TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Waziri wa Nishati Dk. Medard Kalemani akizungumza na watumishi wa Shirika la umeme Tanzania TANESCO Mkoa wa Shinyanga.
Waziri wa Nishati Dk. Medard Kalemani akizungumza na watumishi wa Shirika la umeme Tanzania TANESCO Mkoa wa Shinyanga.
Naibu Waziri wa Nishati Steven Byabato akizungumza kwenye kikao na watumishi wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga.
Kaimu Meneja mwandamizi Rasilimali watu kutoka Shirika la TANESCO Makao Makuu Festo Mkolla, akizungumza kwenye kikao hicho.
Kaimu katibu Tawala mkoa wa Shinyanga Beda Chamatata akizungumza kwenye kikao hicho.
Watumishi wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye kikao chao na Waziri wa Nishati Dk. Medard Kalemani.

Na Marco Maduhu-Shinyanga.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post