Vyombo vya ulinzi na usalama mkoa wa Dar es salaam, vimefanikiwa kuwatia mbaroni wahamiaji haramu 36 raia wa Ethiopia na Somalia walioingia nchini kinyume na taratibu, ambapo mkuu wa mkoa huo Aboubakar Kunenge ametoa onyo kali kwa raia wa Tanzania, wanaoshiriki kuwafadhili na kuwasafirisha ili wapate fedha.
Kunenge amesema Wahamiaji hao walikamatwa usiku wa kuamkia November 15, 2020 kwenye fukwe za Mbweni ambapo kati yao, 30 wanatoka nchini Ethiopia na Sita wanatokea nchini Somalia.
Aidha Kunenge amesema hata utaratibu unaotumika kusafirisha watu hao unakiuka sheria, haki na utu wa binadamu sababu wengi wao wanafungiwa kwenye kontena zisizokuwa na hewa na pindi wanapobainika kufariki Dunia maiti zao hutupwa kwenye vichaka.
Pamoja na hayo RC Kunenge amevipongeza vyombo vya ulinzi na usalama kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya.
Kwa upande wake Afisa uhamiaji mkoa wa Dar Es Salaam, Kamishna Msaidizi Edmund Mrosso amesema kinachofuata baada ya wahamiaji hao kukamatwa watafikishwa mahakamani kwa kosa la Kuingia nchini kinyume na taratibu.
Aidha Kamishna Mroso amesema kwa wale wanaowasafirisha au kuwahifadhi wahamihaji hao, adhabu inaelekeza kifungo cha miaka 20, faini ya shilingi milioni 20 au vyote kwa pamoja ikiwa ni pamoja na kutaifisha mali zilizotumika.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com
🚧🚦 Usiendeshe gari lako bila Mafunzo na Leseni halali_ 📲 Wasiliana nasi sasa: wa.me/255740273285 Unahitaji nini? 🚘 Unataka kujifunza udereva wa magari na kupata Cheti? 📄 Una cheti unataka kupata Leseni? 🔄 Unajua kuendesha lakini huna cheti wala leseni na unataka refresh upate cheti? 🛣️ Una nyaraka zote muhimu lakini unahitaji kujifua zaidi barabarani? ✅ Una Leseni bila cheti na unataka renew? 🌍 Tupo mikoa yote Tanzania hadi vijijini! 📞 Tupigie sasa: 0769 763 285
Social Plugin