WAAJIRI MKOANI ARUSHA WAMESISITIZIWA KUWEKA MIFUMO MADHUBUTI KUWALINDA WAFANYAKAZI


Mgeni rasmi kwenye hafla ya ufunguzi wa Mafunzo ya Vision Zero, Richard Kwitega Katibu tawala Mkoa wa Arusha (Katikati) akiwa na Mkurugezi wa Usalama na Afya Mhandisi Alex Ngata Pamoja na Mkurugenzi wa Mafunzo,Utafiti na Takwimu Ndugu Joshua Matiko
Mhandisi Alex Ngata akiongea kwenye mafunzo ya Vision zero Mkoani Arusha

Baadhi ya Wawakilishi waViwanda,wafanyabiashara,taasisi,kampuni za mkoa wa Arusha wakifuatilia kwa makini, mafunzo ya Vision zero Mkoani Arusha
Baadhi ya Wawakilishi wa Maeneo ya kazi mkoa wa Arusha wakifuatilia kwa makini, mafunzo ya Vision zero Mkoani Arusha 

*********************** 

Mwandishi wetu, Arusha 
Katibu tawala Mkoa wa Arusha Mhe. Richard Kwitega amewasisitiza waajiri mkoani Arusha kuweka mifumo madhubuti ilikuwalinda wafanyakazi dhidi ya magonjwa na ajali katika maeneo yao ya kazi. 

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, kwenye ufunguzi wa mafunzo maalumu ya Vision zero yaliyoandaliwa na Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (OSHA) jijini Arusha, maalamu kwa wamiliki wa meoeo ya kazi mkoa wa Arusha, amesema uwepo wa mifumo mizuri maeneo ya kazi itasidia kuwakinga wafanyakazi dhidi ya magonjwa na ajali zinazotokea maeneo ya kazi. 

Ndugu Richard amesema wafanyakazi ni kipuri namba moja,kwa tassisi au kampuni yeyote katika ufanisi wakazi yeyote, amesema wafanyakazi wana mchango mkubwa sehemu ya kazi hivyo hawana budi kuhakikisha wanawalindwa dhidi ya magojwa na ajali zinazoweza kutokea sehemu za kazi, ilikuwawezesha kufikia malengo waliojiwekea. 

Aidha katibu tawala huyo amesisitiza waajiri kutoa ushirikiano kwa OSHA ilikuhakikisha suala hili linatekelezwa bila vikwazo, amesema wafanyakazi wanamchango mkubwa kwenye suala la usalama na afya mahali pa kazi kwani wao ndio watendaji wa kazi, endapo ushirikiano utakuwepo baina yao, itasaidia kupunguza ajali na magonjwa sehemu za kazi. 

“Suala hili ni la pande tatu yaani mwajiri,mwajiriwa, na serikali naendapo ushirikiano huo utadumishwa basi ajali na magonjwa yatapungua ama kwisha kabisa sehemu za kazi” aliongeza Katibu tawala huyo wa mkoa wa Arusha.

Amewataka wafanyakazi wajenge utamaduni wakujilinda wao wenyewe wakiwa kazini, kwani wao wanabeba jukumu kubwa la kujilinda dhidi ya magonjwa na ajali sehemu za kazi kutokana na majukumu yao ya kila siku.

Akiongea kwa niaba ya Kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA, Mkurugenzi wa Usalama na Afya mhandisi Alex Ngata amesema, Kampeni ya Vision Zero ni kampeni ya kidunia, nchi mbalimbali dunia nizinatekeleza kampeni hii, na lengo kuu la Vision zero ni kupunguza ajali na magonjwa sehemu za kazi. 

Mhandisi Ngata amesema uwepo wa mfumo sehemu za kazi utawawezesha waajiri kujikagua wenyewe, na hivyo kuweza kuzuia magonjwa na ajali sehemu za kazi.

“Mfanyakazi ni msingi imara katika biashara na uzalishaji ambao OSHA unaungalia bila wao hawawezi kuzalisha na kufanyabiashara hivyo ni muhima kuzingatia usalama na afya zao wakiwa kazini ni vema kuwepo na mfumo maeneo yenu ya kazi ilimuweze kulinda nguvu kazi hiyo”.Alisema Mhandisi Ngata.

Kwa upande wao washiriki wa mafunzo hayo wamesema, Vision zero itawasaidia kwenda kuweka mifumo mizuri yakuwalinda wafanyakazi juu ya ajali na magonjwa sehemu za kazi, wamesema mafunzo hayo yamewajengea uelewa mpana juu ya masuala ya usalama na afya, vitu ambavyo walikuwa hawavifahamu.

“Kama mwajiri atatekeleza kama ambavyo vision zero inataka, Kuondoa magonjwa na ajali sehemu za kazi, nakama utafuata maelekezo, natumaini tutazalisha sana sehemu za kazi na hivyo kuongeza pato la taifa, na ukisema umeondoa ajali na magonjwa sehemu za kazi , hata wafanyakazi watakuwa na moyo wakufanya kazi zaidi na pia watakuwa nguvu za kufanyakazi zaidi, tutawashawishi waajiri wetu watekeleze kama ambavyo lengo kubwa la Vision zero linataka”alisema Bwana Emmanuel Mvamila Mwakilishi wa kiwanda cha TPC Moshi. 

Vision zero ni Kampeni ya Kidunia iiliyoanzishwa kwa lengo ya kupunguza ajali na magonjwa sehemu za kazi,kampeni hiyo inazitaka maeneo ya kazi kuweka mifumo ya kuwalinda wafanyakazi dhidi ya magonjwa na ajali sehemu za kazi, na kampeni hii inatekelezwa kwenye mataifa mbalimbali duniani.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post