RAIS WA UGANDA YOWERI MUSEVENI AFUNGUKA KUHUSU UCHAGUZI MKUU WA TANZANIA

Rais wa Uganda Yoweri Museveni, amesema alikuwa anafuatilia kwa makini uchaguzi mkuu wa Tanzania uliofanyika Oktoba 28, 2020, huku akipongeza ulivyoisha kwa amani.

Museveni ameyasema hayo leo kwenye hafla ya kuapishwa kwa Rais Dkt. John Magufuli, ambapo amesema moja ya vitu vilivyomvutiwa ni ushindi wa kishindo wa CCM katika majimbo ya Ilemela pamoja na Hai.

‘Nilikuwa nafuatilia uchaguzi kupitia Television nikaona mama mmoja wa Ilemela ameshinda kwa kishindo, mara nikaona tena Hai nako CCM imeshinda, nikasema sasa kazi nzuri imefanywa na CCM” ,Amesema Museven

“Wengine wanafikiri ni jambo rahisi, lakini Afrika kufaulu lazima tukumbuke jambo la mwelekeo wa kisiasa, baada ya uhuru viongozi wetu waligawanyika,  wengi wa Afrika walichukua mstari wa kuwa vibaraka wa nchi za nje wachache wakiongozwa na mwalimu Nyerere (Julius- Rais wa kwanza wa Tanzania) na wengine kama kina Mzee Kaunda na Seretse Khama walikataa.


"Kama tungefuata mstari ule mwingine wa vibaraka hawa viongozi hawangekuwa hapa,  Kusini ya Afrika yote ilikuwa chini ya wakoloni kwa hiyo mnisamehe kuwa natazama TBC 1 kujua inakwendaje uchaguzi wa 2015 nilikuwa na hofu sana hii imekuwaje? Lakini baadaye nikaona alichaguliwa kwa kura nyingi sana.”

“Safari hii nikaona tena kule Hai nikasema heee Hai, hata Ilemela haya ndiyo majimbo ambayo walitangaza kwanza Newala huko nikasema aah basi, sasa mwisho naona nikiangalia umati wa watu hapa naona vijana wengi sana lakini vijana lazima mrithi msimamo wa wazalendo ambao walitangulia wakiongozwa na Mwalimu Nyerere.”
- Amesema MusevenDownload/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post