RAIS MAGUFULI AWATULIZA WAKUU WA MIKOA NA WILAYA WENYE WASIWASI WA KUTUMBULIWA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na viongozi mbalimbali katika Ikulu ya Chamwino mara baada ya kumuapisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali Profesa Adelardus Lubango Kilangi leo tarehe 09 Novemba 2020. 
***
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli, amewataka watendaji ndani ya serikali kuchapa kazi na kuachana na wasiwasi wa kuhisi atawaondoa.

Magufuli ameyasema hayo leo Novemba 9, 2020 kwenye hotuba yake baada ya kumwapisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali Prof. Adelardus Kilungi Ikulu Chamwino, jijini Dodoma.

"Wakuu wa mikoa na wilaya msiwe na wasiwasi na inawezekana pasitokee mabadiliko yoyote labda kwa atakayestaafu au atakayefanya mambo ya hovyo, kama nilikuteua uwezo si bado ni ule ule najua wananisikia wachape kazi wasipochapa kazi shauri yao'', amesema",amesema Magufuli.

"RC unakuwa na wasiwasi gani labda kama 'performance' yako ilikuwa haifanyi kazi vizuri, nashangaa napata vimeseji kwamba Mh Rais nimejitahidi katika kipindi changu, kana kwamba kipindi chake nilimwambia kinaisha baada ya mimi kuapishwa", - ameongeza Rais Magufuli.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments