RAIS MAGUFULI AITAKIA KILA LA HERI TIMU YA TAIFA STARS DHIDI YA TUNISIA NA BONDIA MWAKINYO | MALUNDE 1 BLOG

Friday, November 13, 2020

RAIS MAGUFULI AITAKIA KILA LA HERI TIMU YA TAIFA STARS DHIDI YA TUNISIA NA BONDIA MWAKINYO

  Malunde       Friday, November 13, 2020


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr John Magufuli amesema  kuwa katika kipindi cha miaka mitano ijayo Serikali itatenga kiasi kidogo cha fedha katika kuziandaa timu mbalimbali za Taifa na pia alitumia fursa hiyo kwa kuitakia heri Taifa Stars kwenye mchezo wake wa leo dhidi ya Tunisia.

 
Dr Magufuli ameyasema hayo leo tarehe 13 Novemba, 2020, wakati wa hotuba ya ufunguzi wa Bunge la 12 jijini Dodoma ambayo ilitoa dira ya uongozi wake katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

“Tutaanza kutenga fedha kidogo kidogo kwa ajili ya kuzianda timu zetu za Taifa na katika hilo napenda kutumia fursa hii, kuitakia heri timu yetu ya Taifa kwenye mechi yao dhidi ya Tunisia hapo baadaye,” alisema Magufuli.

Aidha Rais Magufuli aliongezea kwa kumtakia heri bondia Mtanzania Hassan Mwakinyo ambaye anashuka ulingoni hapo baadaye, kupambana na bondia kutoka nchini Argentina kwenye pambano la raundi 12 la ubingwa wa mabara wa IBF.

“Na pia nataka kumtakia heri mwanamasumbwi wetu, Hassan Mwakinyo anayepambana leo, watanzania tunataka ushindi tumechoka kushindwa,” aliongezea Magufuli.Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post