RAIS CYRIL RAMAPHOSA WA AFRIKA KUSINI AAHIDI KUFUATILIA ILI KUJUA ALIYEMTOROSHA NABII BUSHIRI NA MKEWE | MALUNDE 1 BLOG

Thursday, November 19, 2020

RAIS CYRIL RAMAPHOSA WA AFRIKA KUSINI AAHIDI KUFUATILIA ILI KUJUA ALIYEMTOROSHA NABII BUSHIRI NA MKEWE

  Malunde       Thursday, November 19, 2020


Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesema kuwa kutoroka kwa Nabii wa Malawi na mke wake nchini humo ni jambo ambalo analifuatilia kwa karibu na ameahidi kuchukua hatua baada ya kupata taarifa za kina.

Nabii Shepherd Bushiri na mke wake Mary, wanakabiliwa na mashtaka ya ulaghai na utakatishaji wa fedha nchini Afrika Kusini.

Wawili hao walitoroka nchini Afrika Kusini wiki liyopita na kujisalimisha kwa polisi nchini Malawi baada ya Afrika Kusini kutoa kibali cha kukamatwa kwao.

Kupitia televisheni ya eneo, Rais Ramaphosa amesema tukio la wawili hao kutoroka "halikutakiwa kutokea".

"Bila shaka tutachukua hatua," Rais alijibu alipoulizwa ikiwa serikali inapanga kufanya lolote.

Baadhi ya taarifa zinasema kuwa muhubiri huyo aliyejitangaza mtume pamoja na mke wake walitoroshwa nchi humo kwa njia haramu na genge la watu ambalo linahusika na uuzaji wa magari yaliyoibwa nchini Afrika Kusini na kupelekwa Malawi.

Pia kuna baadhi ya vyombo vya habari Afrika Kusini vilivyosema kuwa nabii huyo alitoroka kwa kutumia ndege ya rais.

Hata hivyo serikali zote mbili zimekanusha madai hayo.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post