OFISI YA ARDHI RUKWA YAWATAHADHARISHA WALIOVAMIA MAENEO YA UMMA


 Na Abdulrahman Salim, Rukwa RS
Ofisi ya Ardhi Mkoa wa Rukwa inaendelea na zoezi la kufanya uhakiki wa maeneo ya wazi na maeneo ya umma yaliyoorodheshwa kwa mujibu wa ramani za mipango miji za halmashauri za mkoa huo ili kubaini endapo kuna uvamizi umefanyika katika maeneo hayo.

Akiongea kuhusiana na zoezi hilo Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Rukwa Swagile Msananga amesema kuwa lengo la kufanya zoezi hilo ni kupata orodha kamili ya meneo ya wazi ili yaweze kutambulika rasmi huku akiwaonya wananchi waliovamia katika maeneo hayo.

“Kwa maeneo ambayo yatakuwa yamevamiwa, kutakuwa hakuna namna ya kufanya isipokuwa wavamizi wataondolewa ili kupisha maeneo ya wazi kwasababu yanatakiwa yalindwe kwa nguvu zote, na maeneo ambayo yapo salama mpaka sasa hivi tutahakikisha mipaka yake inawekwa bayan ana wananchi watatakiwa waiheshimu,” Alisema.

Aidha aliongeza kuwa baada ya kupata orodha ya kamili ya maeneo hayo atakabidhiwa Mkurugenzi ili aweze kuyaandalia hati kwaajili ya ulinzi wa maeneo hayo kwa siku za usoni.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post