MBUNGE MTATURU AWASHUKURU WANANCHI WA SINGIDA MASHARIKI,ATAJA VIPAUMBELE SABA ATAKAVYOANZA NAVYO

Gari la Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Miraji Mtaturu akiwasili katika jimbo hilo kwa ajili ya kuwashukuru wananchi kwa ushindi waliompatia.

MBUNGE wa Jimbo la Singida Mashariki, Miraji Mtaturu,akipokelewa kwa shangwe na mafaruko ya wananchi wake na Chama cha Mapinduzi(CCM) kutoka Bungeni Dodoma,alipowasili jimboni kwake kutoa shukrani za ushindi wa CCM.

MBUNGE wa Jimbo la Singida Mashariki, Miraji Mtaturu,akifurahia na wananchi wake pamoja na Chama cha Mapinduzi(CCM) baada ya kuwasili jimboni humo akitokea Bungeni Dodoma,kwa ajili ya kutoa shukrani kwa ushindi waliompatia kuliongoza jimbo hilo kwa miaka mitano tena.

MBUNGE wa Jimbo la Singida Mashariki, Miraji Mtaturu,akicheza ngoma baada ya kuwasili jimboni humo akitokea Bungeni Dodoma,kwa ajili ya kutoa shukrani kwa ushindi waliompatia kuliongoza jimbo hilo kwa miaka mitano tena.

MBUNGE wa Jimbo la Singida Mashariki, Miraji Mtaturu,akiwa na Mwenyekiti Wilaya ya Ikungi ,Mika Likapakapa wakipiga makofi kwa vikundi vya ngoma (havipo pichani) baada ya kuwasili jimboni humo akitokea Bungeni Dodoma,kwa ajili ya kutoa shukrani kwa ushindi waliompatia kuliongoza jimbo hilo kwa miaka mitano tena.

MBUNGE wa Jimbo la Singida Mashariki, Miraji Mtaturu,akvishwa vitu vya kimila na Wazee baada ya kuwasili jimboni humo akitokea Bungeni Dodoma,kwa ajili ya kutoa shukrani kwa ushindi waliompatia kuliongoza jimbo hilo kwa miaka mitano tena.

MBUNGE wa Jimbo la Singida Mashariki, Miraji Mtaturu,akiwashukuru wananchi wake pamoja na Chama cha Mapinduzi(CCM) kwa kumpatia zawadi mara baada ya kuwasili jimboni humo akitokea Bungeni Dodoma,kwa ajili ya kutoa shukrani kwa ushindi waliompatia kuliongoza jimbo hilo kwa miaka mitano tena.

MBUNGE wa Jimbo la Singida Mashariki, Miraji Mtaturu,akiwa ameshikiria silaha za jadi baada ya kukabidhiwa na Wazee mara baada ya kuwasili jimboni huko akitokea Bungeni Dodoma,kwa ajili ya kutoa shukrani kwa ushindi waliompatia kuliongoza jimbo hilo kwa miaka mitano tena.

Mzee Maarufu Ikungi Bw.Hussein Sungita akitoa neno kwa Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Miraji Mtaturu,(hayupo pichani) baada ya kuwasili jimboni humo akitokea Bungeni Dodoma,kwa ajili ya kutoa shukrani kwa ushindi waliompatia kuliongoza jimbo hilo kwa miaka mitano tena.

Katibu wa Wilaya ya Ikungi Kangaeli Akyoo akizungumza na wananchi waliojitokeza kumpokea Mbunge wao wa Jimbo la Singida Mashariki, Miraji Mtaturu mara baada ya kuwasili jimboni humo akitokea Bungeni Dodoma,kwa ajili ya kutoa shukrani kwa ushindi waliompatia kuliongoza jimbo hilo kwa miaka mitano tena.

Mwenyekiti wa wilaya ya Ikungi Mika Likapakapa akiongea na umati wa wananchi wa wa Jimbo la Singida Mashariki, waliojitokeza kumpokea Mbunge wao Miraji Mtaturu baada ya kuwasili jimboni huko akitokea Bungeni Dodoma,kwa ajili ya kutoa shukrani kwa ushindi waliompatia kuliongoza jimbo hilo kwa miaka mitano tena.

Mama wa Miss Tanzania 2006/07, Wema Isaac Sepetu, Mariam Sepetu

Mama wa Miss Tanzania 2006/07 ,Wema Sepetu,Mariam Sepetu ,akielezea furaha aliyonayo baada ya Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Miraji Mtaturu kuchaguliwa tena kuwa Mbunge na anaamini kuwa ataendelea kuwatumika wananchi mpaka aatakampochoka mwenyewe kuliongoza jimbo hilo.

MBUNGE wa Jimbo la Singida Mashariki, Miraji Mtaturu,akiwahutubia mamia ya wananchi wake pamoja na Chama cha Mapinduzi(CCM) baada ya kuwasili jimboni humo akitokea Bungeni Dodoma,kwa ajili ya kutoa shukrani kwa ushindi waliompatia kuliongoza jimbo hilo kwa miaka mitano tena.

Sehemu ya wananchi wakifatilia hotuba ya Mbunge wao wa Jimbo la Singida Mashariki, Miraji Mtaturu wakati akiwashukuru na kuwapongeza kwa kumpa ridhaa ya kuwatumikia tena miaka mitano mengine mara baada ya kuwasili jimboni huko akitokea Bungeni Dodoma,kwa ajili ya kutoa shukrani kwa ushindi waliompatia kuliongoza jimbo hilo kwa miaka mitano tena.

Na.Alex Sonna,Ikungi Singida

Hivi ndivyo unaweza kusema kuwa ni Mafuriko ya wananchi na wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa Mbunge wao Mhe.Miraji Mtaturu walivyompokea kwa shangwe na furaha baada ya kuwasili katika Jimbo hilo la Singida Mashariki akitokea bungeni Dodoma kwa ajili ya kuwashukuru kwa kumuani tena miaka mitano tena kwa ushindi wa kishindo.

Akizungumza na baada ya kupokelewa na wananchi wake na Chama cha CCM Mhe.Mtaturu amewashukuru wananchi wa jimbo hilo kwa kuendelea kumuamini tena huku akisema kuwa atawatumikia wananchi bila kuwabagua kwa itikadi zao za kisiasa.

Aidha Mtaturu amewambia wananchi kuwa uchaguzi kwasasa umekwisha hivyo wananchi washirikiane kuhakikisha Wilaya ya Ikungi inapata mafanikio na yeye kama kiongozi wao atawatumikia wote bila ubaguzi.

“Tayari Mimi ni Mbunge wenu nipo tayari kushirikiana nanyi, lakini pia tujenge mahusiano, tuachane na itikadi zetu za kisiasa sasa tujenge uchumi wa Jimbo la Ikungi, tumechelewa sana,”amesisitiza

Hata hivyo Mhe.Mtaturu ametaja vipaumbele saba atakavyoanza navyo ikiwemo suala la elimu ambapo atasimamia kuhakikisha watoto wanapata elimu bora,Maji,Umeme,Afya pamoja na miradi iliyopo inatekelezwa na kuibua mingine.

Aidha Mhe.Mtaturu amewahamasisha akinababa kuunda vikundi vya wakulima ili waweze kupata mikopo itakayosaidia kuinua kilimo chao katika wilaya ya Ikungi na pia wataweza kupata mikopo wakiunda vikundi hivyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments