MBOWE NA WENZAKE WAACHIWA KWA DHAMANA | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, November 3, 2020

MBOWE NA WENZAKE WAACHIWA KWA DHAMANA

  Malunde       Tuesday, November 3, 2020

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe ni kati ya viongozi wa upinzani walioachiwa kwa dhamana leo Jumanne Novemba 3, 2020.

Wengine walioachiwa ni wajumbe wa kamati kuu ya Chadema,   Godbless Lema na Boniface Jacob ambao pamoja na Mbowe walikamatwa na polisi usiku wa kuamkia Novemba 2, 2020 wakiwa kwenye kikao. Zitto alikamatwa leo mchana alipokwenda kuwatembelea kina Mbowe polisi.


Wakili wa Chadema John Mallya amesema viongozi hao wameachiwa kwa dhamana na kutakiwa kuripoti polisi Novemba 5, 2020 saa 3 asubuhi.

Mallya amesema viongozi hao wameachiwa baada ya kujidhamini wenyewe na kutakiwa kutotoka nje ya mkoa wa Dar es Salaam na kuhakikisha wanaripoti kituoni hapo tarehe waliyopangiwaUsikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post