ASKOFU GWAJIMA AFUNGUKA KWA MARA YA KWANZA BUNGENI MBELE YA RAIS MAGUFULI

Mbunge wa Kawe kupitia Chama cha Mapinduzi, Josephat Gwajima, kwa mara ya kwanza leo Bungeni kazungumza, ambapo amemshukuru Rais Magufuli kwa kumrahisishia kuingia Bungeni, ambapo pia amemsihi kuendelea kuchapa kazi badala ya kusikiliza kelele za watu wengine.

“Ukiwa unasafiri halafu ukawa unasimama kila mahali kumtupia mawe kila Mbwa anayebweka, hutofika safari yako,  Rais wacha mbwa wabweke tuendelee na safari yetu ya kutimiza ilani ya kurasa 303, waache wabweke kwa raha zao wewe kaza mwendo.

“Sisi wabunge tulioingia Bungeni kwa mara ya kwanza ‘performance’ yako ya miaka mitano iliyopita imetubeba sisi kwenye majimbo yetu na bila shaka tumepata kura kupitia wewe, ulikuwa ndiyo tofali katika ushindi wetu, kuna sehemu hatukuhitaji kupiga kura tulitaja jina lako tu” Gwajima

Aidha, Gwajima amesema wabunge wote walioibuka na ushindi katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 28, 2020 ni ‘majabali’ hivyo itakuwa kazi rahisi kwa Rais John Magufuli kuwateua baadhi yao kuwa mawaziri.

Askofu huyo wa Kanisa la Ufufuo na Uzima ambaye ndio mara yake ya kwanza kuwa mbunge amesema kuwa wabunge wote wako vizuri hivyo itamrahisishia Rais kuunda Serikali.

“Mheshimiwa Rais wabunge wako wote ni majabali, hakuna mbunge mnyonge hata mmoja hapa, na kwa namna hiyo umejipa urahisi wa kutengeneza Serikali yako,” amesema Gwajima.

“Chukua yeyote mheshimiwa atafanya vizuri” amesema Askofu Gwajima huku wabunge wakishangilia kwa kugonga meza na vigelegele, “kwa niaba ya wabunge wenzangu, nataka niseme kwa dhati, sisi wabunge wengine ambao wamekuwepo hapa bungeni kwa muda mrefu tunachukua nafasi hii kukushukuru mheshimiwa Rais tunakushukuru sana.”Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post