TIMU YA WAZIRI MKUU YAKABIDHI MALI ZA SHIRECU ZILIZOPORWA. ..LIMO GHOROFA LA ILALA DAR

 

Mwenyekiti wa timu iliyoundwa na Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa kufuatilia mali za Chama Kikuu cha Ushirika Mkoani Shinyanga (SHIRECU) Asangy Bangu, (kulia), akimkabidhi Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, Hati Saba za viwanja, pamoja na nyumba na ghala, ambazo ni mali tena za SHIRECU zilizokuwa zimeporwa na kuuzwa kinyume na taratibu.

Na Marco Maduhu - Shinyanga. 
Timu ya Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa, iliyoudwa kwa ajili ya kufuatilia mali za Chama Kikuu cha Ushirika mkoani Shinyanga (SHIRECU), ambazo ziliporwa na kuuzwa kinyume na utaratibu, imekabidhi baadhi ya mali na kumilikiwa tena na chama hicho.

Akikabidhi Hati za viwanja, pamoja na nyumba na ghala leo, Mwenyekiti wa timu hiyo Asangy Bangu, amesema wamefanikiwa kurudisha viwanja saba vilivyopo mkoani Shinyanga, nyumba ghorofa tatu ambayo ipo Ilala, pamoja na ghala lililopo Kurasini Jijini Dar es salaam, ambazo ni mali za Chama Kikuu cha Ushirika (SHIRECU). 

Amesema zoezi hilo la kufuatilia mali hizo za SHIRECU, walilifanya kwa kupitia nyaraka za chama hicho,pamoja na kuhoji watu ambao walikuwa wameuziwa wakiwamo watumishi wa Serikali na watu binafsi, na kufanikiwa kukomboa viwanja hivyo saba, ghala, pamoja na nyumba na kwamba wanaendelea kufuatilia mali zingine. 

"Leo tunakabidhi hati saba za mali za Chama Kikuu cha Ushirika (SHIRECU), ambazo ziliuzwa kinyume na taratibu, kuwa rasmi mali za chama hiki tena, na zoezi hili litakuwa endelevu ili kurudisha mali zote," amesema Bangu. 

Naye Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya, ameipongeza timu hiyo kwa kufanya kazi kwa uzalendo, ambayo ilikuwa na mizengwe mingi, huku akiutaka uongozi wa SHIRECU, kuzitunza mali hizo na zisiweze kurudi tena mikononi mwa watu binafsi. 

Amesema zoezi hilo la kufuatilia mali za Chama Kikuu cha Ushirika mkoani Shinyanga (SHIRECU), pamoja na vyama vingine ikiwamo Nyanza cha Jijini Mwanza, na KNCU cha Kilimanjaro, lilianza mwaka 2016, ambapo Rais Magufuli aliagiza mali hizo zifuatiliwe, ndipo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akaunda timu ya kufuatilia mali za vyama hivyo.

Ameongeza kuwa Jijini Mwanza tayari jana wameshakabidhi mali za Nyanza, na sasa wanaelekea mkoani Kilimanjaro kukabidhi mali za KNCU.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, ametaka watu ambao waliuza mali hizo za SHIRECU na kuisababishia hasara kubwa wawajibishwe, ili kuwa mfano kwa watumishi wengine ambao siyo waaminifu na kuuza mali za umma. 

Pia amekitaka chama hicho baada ya kupata mali hizo, kijiendeshe kibiashara pamoja na kukuza miradi yao kuinuka kiuchumi, ikiwamo na Shule ya Sekondari Buluba, kurudi kwenye hadhi yake ya kufaulisha wanafunzi kwa kuajiri walimu wazuri. 

Aidha Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika (SHIRECU), mkoani Shinyanga Lenis Jishanga, ameishukuru timu hiyo kuwarudishia mali zao, na kuahidi kuzitunza pamoja na kujiendesha kibiashara zaidi. 

TAZAMA PICHA HAPA CHINI

Mwenyekiti wa timu iliyoundwa na Waziri Mkuu kufuatilia mali za SHIRECU Asangy Bangu akitoa taarifa namna walivyofanikiwa kukomboa mali za chama hicho, likiwamo Ghorofa la Ilala Jijini Dar es salaam.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, akizungumza kwenye makabidhiano ya mali za SHIRECU.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya, akizungumza kwenye makabidhiano ya mali za SHIRECU.
Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika mkoani Shinyanga (SHIRECU), Lenis Jishanga, akishukuru kupata mali hizo na kuahidi kuzitunza. 
Mwenyekiti wa timu iliyoundwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kufuatilia mali za Chama Kikuu cha Ushirika Mkoani Shinyanga (SHIRECU) Asangy Bangu, (kulia), akimkabidhi mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, hati saba za viwanja, pamoja na nyumba na ghara, ambazo ni mali tena za SHIRECU zilizokuwa zimeporwa na kuuzwa kinyume na taratibu.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, wa pili kushoto, akimkabidhi katibu mkuu wizara ya Kilimo Gerald Kusaya, hati Saba za viwanja, nyumba na ghala, ambazo ni mali rasmi tena za Chama Kikuu cha Ushirika mkoani Shinyanga (SHIRECU), wa kwanza kushoto ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya, meza kuu akimkabidhi Mwenyekiti wa (SHIRECU) Lenis Jishanga, Hati saba za viwanja, nyumba na ghala, ambazo ni mali tena za chama hicho, wa kwanza kushoto ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, kushoto, akishikana mkono na mwenyekiti wa SHIRECU Mkoa wa Shinyanga Lenis Jishanga, mara baada ya kukabidhiwa mali za SHIRECU, ambazo ziliuzwa kinyume na utaratibu.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, kushoto, akishikana mkono na mwenyekiti wa SHIRECU Mkoa wa Shinyanga Lenis Jishanga, mara baada ya kukabidhiwa mali za SHIRECU, ambazo ziliuzwa kinyume na utaratibu
Wajumbe wakiwa kwenye makabidhiano ya mali za chama kikuu cha ushirika mkoani Shinyanga (SHIRECU), ambazo ziliuzwa kinyume na utaratibu.
Wajumbe wakiwa kwenye makabidhiano ya mali za chama kikuu cha ushirika mkoani Shinyanga (SHIRECU), ambazo ziliuzwa kinyume na utaratibu.
Wajumbe wakiwa kwenye makabidhiano ya mali za chama kikuu cha ushirika mkoani Shinyanga (SHIRECU), ambazo ziliuzwa kinyume na utaratibu.
Wajumbe wakiwa kwenye makabidhiano ya mali za chama kikuu cha ushirika mkoani Shinyanga (SHIRECU), ambazo ziliuzwa kinyume na utaratibu.
Wajumbe wakiwa kwenye makabidhiano ya mali za chama kikuu cha ushirika mkoani Shinyanga (SHIRECU), ambazo ziliuzwa kinyume na utaratibu.
Wajumbe wakiwa kwenye makabidhiano ya mali za chama kikuu cha ushirika mkoani Shinyanga (SHIRECU), ambazo ziliuzwa kinyume na utaratibu.
Picha ya pamoja baada ya kumaliza zoezi la kukabidhi mali za Chama Kikuu cha Ushirika mkoani Shinyanga (SHIRECU).

Na Marco Maduhu- Shinyanga.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post