YANGA WAIBANA MBAVU SIMBA UWANJA WA MKAPA

Mabingwa watetezi Simba chini ya Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck leo, Novemba 7,2020 wamebanwa mbavu Uwanja wa Mkapa wakiwa na nyota wao namba moja Clatous Chama.

Yanga ilianza kupata bao la kwanza kupitia kwa Michael Sarpong dakika ya 31 kwa penalti baada ya Tusisila Kisinda kuchezewa faulo nje kidogo ya 18 na nyota Joash Onyango na mwamuzi Abdalah Mwinyi Mkuu kuamua ipigwe penalti kipindi cha pili.


Yanga kipindi cha pili walianza kwa kasi ila beki kisiki Lamine Moro alishindwa kumaliza dakika 90 baada ya kupata maumivu ya goti.

Nafasi yake ilichukuliwa na Said Juma ambaye alishuhudia bao la kwanza kwa Simba dakika ya 86 kwa pasi ya Luis Miquissone ambaye alikuwa ni mwiba kwa wapinzani.

Matokeo hayo yanaifanya Simba kubaki nafasi ya tatu ikiwa na pointi 20 huku Yanga ikiwa nafasi ya pili na pointi zake 24 na vinara ni Azam na pointi zao ni 25.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post