MBUNGE RIDHIWANI KIKWETE AFANYA ZIARA TARURA-CHALINZE, AAHIDI KUPIGANIA KUONGEZA BAJETI ZAIDI


Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akizungumza na Meneja wa TARURA- Chalinze, Mhandisi Enrico Shauri (kulia).
Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete ameendelea na ziara maalum ambapo leo ametembelea ofisi za Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini-Tanzania (TARURA)- Chalinze ili kuona namna wanavyofanya kuendelea kuboresha miundombinu ya barabara korofi za Halmashauri hiyo.

Awali akifanya mazungumzo na Meneja wa TARURA- Chalinze, Mhandisi Enrico Shauri leo, Mbunge Ridhiwani alitaka kufahamu mpango mkakati wa namna ya kuboresha baadhi ya barabara zilizo katika Kata hiyo ambazo zimekuwa kero kwa kipindi kirefu.

"Chalinze tuna barabara nyingi lakini baadhi ya barabara hizo zina usumbufu mkubwa hasa baada ya wakati wa mvua hazipitiki kirahisi; je Tarura tumejipangaje na ni kwa namna zitakavyokuwa zinapitika muda wote.?"

Pamoja na hoja hiyo Mheshimiwa Mbunge alitamani kujua wamejipangaje kufungua baadhi ya barabara ambazo zikifunguliwa zitakuwa msaada mkubwa kwa Wananchi wa Chalinze kufikia malengo.

Kwa upande wake Meneja wa TARURA- Chalinze, Mhandisi Enrico Shauri alianza kwa kupongeza ziara hiyo ya Mbunge ambapo pia aliahidi kuyafanyia kazi maagizo na ushauri wote  uliotolewa kayoka mazungumzo yao.

Mhandisi Shauri alieleza changamoto kubwa wanayokabili ni ufinyu wa Bajeti ambao unasababisha ufanisi wa kazi zao kusuasua" akifafamua Muhandisi Shauri alisema kuwa TARURA- Chalinze ina kilometa (KM) 679 ambazo ni nyingi sana kwa bejeti inayotengwa ya mfuko wa barabara ni  Milioni 700.44. 

Kwa mwaka huu 2020-2021 tumeshapewa milioni 200 na zingine zitaendelea kutolewa kwa awamu.utolewaji wa haraka wa mafungu ndiyo utawezesha kukamilika kwa kazi mapema.

Mh. Mbunge alimuahidi Meneja wa Tarura kwenda kushauriana na madiwani wenzake kwa kujenga hoja ili aongezewe mafungu ili kuwezesha ujenzi wa Miundo mbinu ya Halmashauri ufanyike haraka kwa faida ya Maendeleo ya Chalinze na Tanzania kwa jumla.

Kwa upande wa Mh. Mbunge alimshukuru Mkandarasi na Tarura kwa jinsi walivyojitahidi kujenga miundombinu pamoja na changamoto hiyo ya kibajeti.

Pamoja na kusikia toka Tarura, Mh.Mbunge alitumia nafasi hiyo kuhimiza maandalizi ya marekebisho na ujenzi wa barabara korofi zote za halmashauri zikiwemo zile za kata ya Kimange, Miono, Mkange, Vigwaza, Ubena, Talawanda, Mandela, Mji wa Chalinze na maeneo mengine kama sehemu za kutolewa macho sana kutokana na shughuli za kimaendeleo na kuchangia uchumi katika Halmashauri hiyo.

Mheshimiwa Mbunge alimaliza kwa kuwaahidi Ushirikiano mkubwa ili kufikia malengo makubwa waliyopanga kuyasimamia kwa pamoja wakishirikiana na Wananchi.

Ziara ya Kata kwa kata inaanza Jumatatu tarehe 30 ambapo Mbunge anatarajia kwenda kata Kata kukagua miradi ya Maendeleo na kuzungumza na Wananchi kusikia kero na matarajio waliyonayo kwa Serikali yao inayoongozwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments