SHIRIKA LA OPE LATOA PEMBEJEO ZA KILIMO KUHAMASISHA ZAO LA MTAMA WILAYANI KISHAPU
 Na Marco Maduhu, Kishapu.

Shirika lisilokuwa la kiserikali la Organization of People Empowerment (OPE) la Mkoani Shinyanga, limetoa msaada wa Pembejeo za kilimo kwa wananchi wa Kata ya Busangwa wilayani Kishapu, kwa ajili ya kuhamasisha kilimo cha zao la Mtama.

Zoezi la ugawaji wa pembejeo hizo za kilimo, limefanyika leo eneo la Shule ya Msingi Ng’wajipugila Kata ya Busangwa, na kuhudhuliwa na mgeni rasmi afisa kilimo wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu George Kesyy, akimwakilisha Mkurugenzi wa halmashauri hiyo.

Afisa miradi kutoka Shirika hilo la OPE, Joseph Kasya, amesema Pembejeo hizo wamezitoa katika vikundi vinne, ambavyo vilipewa mafunzo kwa ajili ya kulima mashamba darasa ya zao la Mtama, ambayo yatakuwa chachu kwa wakulima kwenye Kata hiyo ya Busangwa, na hatimaye kulima kilimo chenye tija na kupata mavuno mengi.

“Shirika la OPE tumepokea Ruzuku kutoka Shirika la Tanzania Development Trust (TDT) la uingereza, kwa ajili ya kuingia ubia na jamii katika kuhamasisha kilimo cha zao la Mtama, ili kuongeza upatikanaji wa chakula cha kutosha kwa wananchi”, amesema Kasya.

“Katika mradi huu tumetoa mafunzo kwa wakulima kutoka vikundi Vinne vya Kata ya Busangwa, ili wakalime mashamba darasa ya zao la Mtama, na kufundisha wenzao namna ya kulima zao hili kisasa, na leo tumekuja kutoa Pembejeo kwa ajili ya kuwezesha wananchi kulima Mtama, ambapo tumetoa mbegu bora kabisa pamoja na majembe,”ameongeza.

Naye mgeni huyo Rasmi afisa kilimo wilayani Kishapu George Kessy, amelipongeza Shirika hilo kwa kushirikiana na Serikali, kuhamasisha wananchi kulima mazao ambayo yanasatahimili ukame, ili wapate mavuno mengi na kuondokana na baa la njaa hapo baadae.

Amesema ni vyema wananchi wilayani Kishapu katika msimu wa kilimo wa mwaka huu (2020-2021), wakajikita kulima mazao ambayo yanastahimili ukame, kutokana na taarifa za hali ya hewa kuwa hakutakuwa na mvua za kutosha , hivyo ni vyema wakaanza kuchukua tahadhari mapame na kulima mazao hayo.

Ametaja mazao pendekezwa ambayo yanastahimili ukame na kulimwa kwenye ardhi ya Kishapu, kuwa ni Mtama, Choroko, Dengu, Alzet, Viazi Lishe, vitamu, pamoja na mazao ya biashara Pamba na Mkonge.

Nao baadhi ya wanufaika na pembejeo hizo akiwamo Rebeka Ruchagula, ameshukuru kwa kupewa mafunzo hayo ya kilimo cha kisasa cha zao la Mtama pamoja na Pembejeo, na kuahidi kwenda kulima zao hilo na kutoa elimu kwa wenzao ili wanufaike na kupata mavuno mengi.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI

Afisa miradi kutoka Shirika la OPE Joseph Kasya, akizungumza kwenye makabidhiano ya Pembejeo kwa vikundi vinne vya Shamba darasa kwa ajili ya kulima zao la Mtama Kata ya Busagwa wilayani Kishapu.

Mgeni Rasmi Afisa kilimo wilayani Kishapu George Kessy, akizungumza kwenye makabidhiano ya Pembejeo kwa vikundi vya Shamba Darasa la zao la Mtama Kata ya Busangwa wilayani humo.
Afisa kilimo wilyani Kishapu George Kessy, akisisitiza wananchi wote wilayani humo, kuwa mwaka huu wajikite kulima Mazao yanayostahimili ukame.
Wanavikundi wa kilimo cha zao la Mtama kutoka Kata ya Busangwa wilayani Kishapu, wakiwa kwenye zoezi la kukabidhiwa Pembejeo za kilimo kwa ajili ya kulima zao hilo la Mtama kwenye Mashamba darasa.

Afisa kilimo halmashauri ya wilaya ya Kishapu George Kessy. (kulia) akikabidhi Pembejeo za kilimo ili kuhamasisha kilimo cha zao la Mtama.
Zoezi la kukabidhi Pembejeo likiendelea.

Zoezi la kukabidhi Pembejeo likiendelea.
Zoezi la kukabidhi Pembejeo likiendelea.
Pembejeo, ambazo ni Majembe, na Mbegu za zao la Mtama zikiwa ndani ya mfuko.

Picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa zoezi la kukabidhi Pembejeo kwa wakulima.
Picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa zoezi la kukabidhi Pembejeo kwa wakulima.

Na Marco Maduhu- Kishapu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post