BABA ASAKWA KWA KUMUUA MTOTO WAKE


Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linamsaka baba mzazi, Adam Athuman (30-40) kwa tuhuma za kumuua mtoto wake mwenye umri wa miaka 10 Adam Athuman aliyekuwa mwanafunzi wa darasa la tatu shule ya msingi Nyamadoke Kata ya Buswelu Wilaya ya Ilemela. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, ACP Muliro Jumanne amesema  limetokea Novemba 22, 2020 majira ya saa 5:30 katika Kata ya Buswelu wilayani Ilemela ambapo mtoto huyo aliuawa kwa kushambuliwa na fimbo sehemu za mwili wake.

TAREHE 22.11.2020 MAJIRA YA 11:30HRS HUKO KATA YA BUSWELU, WILAYA YA ILEMELA, ATHUMAN ADAM,  MIAKA 10, MKEREWE, MWANAFUNZI WA DARASA LA TATU, SHULE YA MSINGI NYAMADOKE, BUSWELU, ALIUAWA KWA KILE KICHODAIWA KUSHAMBULIWA NA FIMBO SEHEMU ZA MWILI WAKE NA BABA YAKE MZAZI ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA ADAM ATHUMAN, MIAKA KATI YA 30-40, MKEREWE, FUNDI UJENZI, NYAMADOKE, MTUHUMIWA HUYO BAADA YA KUTEKELEZA UKATILI  HUO ALITOROKA, NA JESHI LA POLISI  LINAFANYA KILA JITIHADA KUHAKIKISHA ANATIWA  NGUVUNI  ILI AFIKISHWE KWENYE VYOMBO VYA SHERIA. MWILI WA MAREHEMU UMEFANYIWA UCHUNGUZI HOSPITALI YA BUGANDO NA KUKABIDIWA NDUGU KWA MAZISHI.

JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINAWAONYA NA KUTOA WITO KWA WAZAZI NA WALEZI WOTE KUWA MAKINI NA AINA YA ADHABU WANAZOTOA KWA WATOTO, KWANI WANAWEZA KUJIKUTA WAKITENDA MAKOSA YA KIJINAI NA HATIMAYE KUFIKISHWA MAHAKAMANI. 

IMETOLEWA NA;

Muliro JUMANNE MULIRO – ACP

KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA

25, NOVEMBA 2020

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments