WANAFUNZI 3,941 HALMASHAURI YA WILAYA YA MBULU KUHITIMU DARASA LA SABA


Na John Walter- Mbulu
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya  wilaya ya Mbulu Hudson Kamoga amesema watahiniwa 3,941 wakiwamo wasichana 2,198 na wavulana 1,743 wanatarajiwa kufanya mitihani ya taifa ya kuhitimu darasa la saba Oktoba 7 hadi 8,2020.Akizungumza na waandishi wa habari, amesema wanafunzi wote hao  wapo  tayari kwa ajili ya mtihani huo wa Taifa.

Kamoga   amesema  kuwa mitihani hiyo itafanyika kwa siku mbili  (Jumatano na  na alhamisi ) na mpaka sasa taratibu zote zimeshakamilika na serikali imeshatoa  fedha zote zinazohitajika kwa ajili  ya zoezi hilo.

Amesema wahitimu hao wote ni wanufaika wa matunda ya Elimu bila malipo ambapo serikali katika Halmashauri ya wilaya ya Mbulu ilitoa shilingi Bilioni 4.9 ambazo Bilioni  3.5 zilihudumia Shule za Msingi na Bilioni 1.4 katika Shule za Sekondari tangu mwaka 2016 ilipoanza Elimu ya msingi na Sekondari bila malipo ambapo wanafunzi hao walikuwa darasa la tatu.

Ametoa wito  kwa wazazi/walezi kuhakikisha wanawahimiza watoto wao kufika kwa wakati kufanya mtihani huo muhimu na ni kosa kisheria kumzuia mwanafunzi kufanya mtihani.


Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527