SHULE YA AFRICAN MUSLIM YATEKETEA KWA MOTO

Bweni la shule ya sekondari ya Kiislam ya African iliyoko maeneo ya Kaloleni mkoani Kilimanjaro, limeteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo Oktoba 9, 2020, na kwamba hii ni mara ya tatu kwa shule hiyo kuungua.


Akizungumza leo Oktoba 9, 2020, Mkaguzi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Kilimanjaro, Inspekta Jeremiah Mkomagi, amesema kuwa walipata taarifa za moto huo majira ya saa 1:40 usiku na mpaka wanafika eneo la tukio moto ulikuwa umeshika sehemu kubwa ya bweni.

"Tulipata wito kwamba kuna moto katika shule ya sekondari ya African Muslim na tulipofika tukakuta moto ni mkubwa sana na ni jengo la bweni la ghorofa moja na moto ulikuwa umeanzia kwenye moja ya chumba ambacho kinatumika kama stoo", amesema Inspekta Jeremiah.

Aidha Inspekta Jeremiah ameongeza kuwa "Kwenye tukio hilo hakuna majeruhi wala kifo kwa sababu wanafunzi waliondolewa mapema na kupelekwa sehemu salama, vitu vilivyoungua ni nguo zao, vitanda na madaftari, chanzo hakijabainika kwa sababu kumekuwa na mlolongo wa shule kuungua na hii ni mara ya tatu".




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments