Polisi Wamkamata na Kumwachia Halima Mdee

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni asubuhi ya leo Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020 walimkata Mgombea Ubunge wa Kawe, Halima Mdee wa Chadema kufuatia sintofahamu iliyojitokeza katika zeozi la upigaji kura jimboni humo.

 Taarifa zinaeleza, Mdee alikamatwa katika Kituo cha Kawe kufuatia sintofahamu hiyo kutokea baada ya mgombea huyo kudai kuona masanduku ya kura yakiwa na kura zilizopigwa kinyume na utaratibu.

Akizungumzia sakata hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Edward Bukombe amesema, mgombea huyo alihojiwa baada ya kukamatwa kisha akaachiwa huru.

Kuhusu madai ya Mdee ya sanduku kukutwa na kura feki, Kamanda Bukombe amesema hawajapokea taarifa hizo.

.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments