"NILETEENI KIMEI”.....RAIS MAGUFULI AWAAMBIA VUNJO


 Rais John Magufuli ambaye ni Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, amewaasa wananchi wa jimbo la Vunjo kutofanya makosa ya kutompa kura mgombea ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya CCM, Dkt.Charles Kimei, kama wanataka maendeleo ya ukweli.  

Akizungumza na Wanachi wa mji mdogo wa Himo uliopo katika Wilaya ya Moshi vijini, jimbo la Vunjo, Rais Magufuli amesema kuwa Dokta Kimei ni mchapakazi asiye na maneno mengi, lakini amafenya mengi katika nafasi alizohudumu, kuanzia Benki Kuu ya Tanzania na hatimaye Benki ya CRDB. 
 
“Nileteeni Dokta Kimei, huyu Kimei mimi namjua vizuri. Alifanya kazi nzuri Benki Kuu ya Tanzania na akaleta mabadiliko makubwa sana ndani ya Benki ya CRDB pamoja na kusaidia mikoa mbalimbali, ikiwemo Mkoa huu wa Kilimanjaro. Pia amebuni na kusaidia  miradi iliyogusa wananchi wa kawaida. Nitashangaa kama hamtapa kura. Ili tupige hatua za maendeleo, Bunge letu linahitaji watu wa aina ya Dokta Kimei. Nileteeni Kimei” alisema Rais Magufuli.

Akijibu ombi la Dokta Kimei kuhusu kuomba kuanzishwa kwa Wilaya ya Vunjo ambayo itakuwa na Makao Makuu yake katika mji wa mdogo wa Himo, ili kuongeza ufanisi, mapato ya serikali na utawala bora, Rais Magufuli alisema kuwa jambo hili liko ndani ya uwezo wake na kuwasihi wananchi wa Vunjo kumchagua Dkt.Kimei na Madiwani wote 16 ili walisimamie na hatimaye kulifanikisha jambo hilo la msingi.

Kuhusu changamoto ya barabara za kimkakati ikiwemo ile ya Kilema na ya soko la Vunjo. Rais Dokta Magufuli alisaema kuwa suala la ujenzi wa mioundo mbinu liko ndani ya ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi na atahakikisha lianfanyiwa kazi haraka iwezekanavyo.

Rais Magufuli anaendelea na ziara yake Mkoani Kilimanjaro ambapo  leo atakuwa na Mkutano mkubwa wa kampeni katika Uwanja wa Ushirika mjini Moshi.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments