MBUNGE MTEULE NEEMA AFANYA ZIARA KATIKA MASOKO AKUTANA NA WANAWAKE WAJASIRIAMALI

 

MBUNGE Mteule wa Viti Maalumu CCM (NGOs) Tanzania Bara Neema Lugangira kulia akipokea maoni ya wanawake wanaouza mbogamboga sokoni juu ya namna ya kuwaboreshea mazingira ya kazi
Mama mwenye mtoto ambaye bado ana mnyonyesha akitoa maoni yake kwa Mbunge Mteule wa Viti Maalumu CCM (NGOs) Tanzania Bara Neema Lugangira juu ya uhitaji wa mazingira wezeshi sokoni ambayo ilani ya CCM 2020-2025 imesema
Mbunge Mteule wa Viti Maalumu CCM (NGOs) Tanzania Bara Neema Lugangira kulia akimuelewesha mama mjasiriamali juu ya umuhimu wa kupiga kura
Mama mwenye mtoto ambaye anamnyonyesha akisikiliza kwa umakini ilani ya CCM 2020-2025 imesema nini kuhusu wanawake wajasiriamali wadogo masokoni na wenye watoto wadogo

MBUNGE Mteule wa Viti Maalumu CCM (NGOs) Tanzania Bara Neema Lugangira kulia akijadiliana na wanawake wanaouza mboga sokoni juu ya changamoto zao
 
MBUNGE Mteule wa Viti Maalumu CCM (NGOs) Tanzania Bara Neema Lugangira amefanya ziara katika masoko ya Kashai, Rwamishenye na Soko Kuu ili kuweza kujadiliana na wanawake wajasiriamali kwa lengo la kuona namna ya kuboresha miundombinu ili waweze kuuza bidhaa zao kwa usalama

Wajasiriamali ambao amekutana nao ni wanawake wanauza mbogamboga ikiwa ni muendelezo wa kampeni zake za kisayansi ili kuweza kuona namna nzuri ya kuweza kuboresha miundombinu hiyo na kuwaondolea kero.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mbunge Mteule Neema alisema suala la usalama katika eneo la kuuza mboga mboga sokoni ni jambo muhimu sana kwani litapelekea kuhakikisha viini lishe havipotei.

Alisema pia sambamba na hilo walijadiliana na wanawake sokoni wenye watoto wanaonyonyeshwa ili kuona namna ya kuweka mazingira rafiki ili watoto waendelee kupata uhakika wa lishe bora wakati mama zao wakiwa kazini.

Hata hivyo wanawake hao wajasiriamali kwenye masoko ya Rwamishenye, Kashai na Soko Kuu walielimishwa juu ya sababu za kuipigia kura CCM na walipata elimu ya mpiga kura na kusisitizwa Oktoba 28 kujitokeza kwa wingi.

“Lakini pia ndugu zangu wajasiriamali tuhakikishe tunampa kura nyingi za kishindo Mhe Rais Dkt John Magufuli kwani amefanya kazi kubwa na nzuri kwa kuwapa maendeleo watanzania hususan sisi wanawake “Alisema Lugangira


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments