MAALIM SEIF KUIFANYA ZANZIBAR KUWA KITUO KIKUU CHA MAWASILIANO DUNIANI AKISHINDA UCHAGUZI | MALUNDE 1 BLOG

Sunday, October 4, 2020

MAALIM SEIF KUIFANYA ZANZIBAR KUWA KITUO KIKUU CHA MAWASILIANO DUNIANI AKISHINDA UCHAGUZI

  Malunde       Sunday, October 4, 2020

Mgombea Uras wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha ACT Wazalendo Malim Seif Sharif Hamad amesema endapo atachaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar anadhamiria kuifanya Zanzibar kuwa kituo kikuu cha mawasiliano duniani ikiwa pamoja na kuijenga bandari ya Wete na Mkoani.

Malimu Seif ametoa ahadi hiyo kwenye mkutano wa kampeni zake kisiwani Pemba kuomba kura kwa wananchi wa Pemba wamchague kuwa Rais wa Zanzibar katika uchaguzi mkuu ujao.

Aidha, amesema endapo atachaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar atawafutia deni la elimu ya juu Wazanzibar wanalodaiwa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu waliosoma kwa mkopo wanaoendelea kudaiwa na bodi hizo za mikopo.

Amesema amerejea Unguja bada ya kumaliza awamu ya pili ya kampeni kisiwani Pemba kuomba ridhaa ya wananchi wa Pemba kumchagua, baada ya kufanya mikutano Mauwani kiwani Pujini jimbo la Chonga, Mapofu Wingwi na kumalizia kijijini kwake jimbo la Mtambwe.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post