KUELEKEA UCHAGUZI MKUU VIONGOZI WA DINI MKOA WA TANGA WAKUTANA WATOA MAAZIMIO

 

SHEHE wa Mkoa wa Tanga Juma Luwuchu akizungumza wakati wa kikao hicho kulia Mwenyekiti wa umoja wa Makanisa Tanga Askofu Dr Jotham Mwakimage
SHEHE wa Mkoa wa Tanga Juma Luwuchu akizungumza wakati wa kikao hicho kulia Mwenyekiti wa umoja wa Makanisa Tanga Askofu Dr Jotham Mwakimage
Mwenyekiti wa umoja wa Makanisa Tanga Askofu Mstaafu wqa Kanisa la TAG Dr Jotham Mwakimwage  
Kamanda wa polisi Mkoa wa Tanga Blasius Chatanda kulia akifuatilia matukio mbalimbali kwenye kikao hicho
FR Richard Kimbu wa Kanisa Katoliki Mkoa wa Tanga akichangia jambo kwenye mkutano huo kushoto ni FR Severine Msigiti wa RC Tanga na kulia ni Fr Martin Maganga wa Kanisa Katoliki Mtakatifu Theresia Tanga
MCHUNGAJI wa Kanisa la Waadiventist Wasabato lililopo Kana Jijini Tanga, Jackson Mdingi akichangia jambo wakati wa kikao hicho kulia ni Shehe wa Mkoa wa Tanga Juma Luwuchu kushoto ni Mjumbe wa Baraza la Mashehe Mkoa wa Tanga Shehe Juma Bakari
Mjumbe wa Baraza la Mashehe Mkoa wa Tanga Shehe Juma Bakari akisistiza jambo wakati wa kikao hicho


KUELEKEA Uchaguzi Mkuu Octoba 28 mwaka huu kamati ya viongozi wa dini mkoani Tanga wamekutana huku wakitoa maazimio matano ikiwemo kupinga aina yoyote ya vurugu na maandamano, viashiria vya uvunjifu wa amani vinavyoweza kujitokeza wakati wa uchaguzi huo.

 

Akisoma maazimio ya Baraza la Amani mkoa wa Tanga Askofu Mstaafu wa Kanisa la TAG Dkt Jonson Mwakimwage wakati wa kikao cha Baraza hilo ambacho kiliketi kwenye ukumbi wa Tanga Beach Jijiji Tanga.

 

Alisema wao kama viongozi wa dini hawatakubali kuona vurugu na maandamano yakitokea wakati wa uchaguzi huo badala yake watakuwa mstari wa mbele kuhakikisha vitendo vya namna hiyo havitokei kwenye jamii ili watanzania waweze kushiriki kwa amani kwenye uchaguzi huo

 

“Leo viongozi wa dini mkoani Tanga tumekutana kwenye kikao hiki maalumu kuelekea kwenye uchaguzi mkuu lakini moja ya maazimio yetu ni kutaka uchaguzi kufanyika kwa amani na tunakataa maandamano ya vurugu ya aina yoytote”Alisema Askofu Mwakimage.

 

Alisema wao kama baraza hilo wanakataa na kutokuuunga mkono vitendo vya maandamano na vurugu aina yoyote ikiwemo viashiria vya matamshi vinavyoashiria uvunjifu wa amani hawavikubaki

 

Askofu huyo alisema kwamba wao kama kamati ya amani mkoa wameyakataa na hawataridhia watu wenye matamshi mabaya ya kuvuruga amani wakati wa uchaguzi huo huku wakieleza watakaochaguliwa watakubaliana nao na kuwaunga mkono

 

 Awali akizungumza wakati wa kikao hicho Shehe wa Mkoa wa Tanga Juma Luwuchu alisema wao viongozi wa dini wana kazi kubwa ya kuhakikisha waanatakiwa kuwa mstari wa mbele kuhimizxa amani,

 

Alisema kwamba moto mkubwa mkubwa chanzo chake ni cheche hivyo wakichezea cheche ya moto wananchi kwa sababu uchaguzi ni siku moja na maisha ni kile siku hivyo walitambue hilo na kufikiria.

 

“Ndugu zangu tusichezee cheche wakati wa uchaguzi kwani siku moja tukichezea tunaweza kufanya tusiwe na nyumba ya kuwaongoza watu misikitini wala makanisani”Alisema Shehe Luwuchu.

 

Aliwataka viongozi wa dini wasigeuke kuwa wapembe wa wanasiasa badala yake wahakikisha wanatumia nafasi zao kuendelea kuihubiri amani na utulivu uliopo hapa nchini

 

“leo kumejitokeza baadhi ya viongozi wanaojiita ni wa dini wanatamka waziwazi na kutamka baadhi ya vyama kwamba hivi ndio vyama na kuhamasisha vijana kujitokeza barabarani hiyo sio dini yetu inavyoelekeza huku wengine wakisema baada ya kura waendelee kukaa vituoni huo sio utaratibu wa dini”Alisema

 

KamaKamanda wa polisi Mkoa wa Tanga Blasius Chatanda ameonya watu au Kikundi Cha watu ambacho kitajaribu kufanya uvunjifu wa amani katika uchaguzi Mkuu ujao kuwa watachukuliwa hatua kali za kisheria.

 

Kauli hiyo aliitoa wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu mikakati iliyowekwa na Jeshi hilo kuelekea katika zoezi la uchaguzi Mkuu.

 

Alisema Kuwa Jeshi hilo limejipanga kuhakikisha zoezi la upigaji Kura hadi kutangazwa kwa matokeo linakuwa la salama na amani.

 

"Niwaambie waliotakaojaribu kuingia mitaani na kufanya maandamano Basi niwaambie watakiona kitakacho watokea kwani tumejipanga kweli kweli safari hii"alisema RPC Chatanda.

 

Aidha aliwataka wananchi kuendelea kutoa taarifa za kuwepo vitendo vya viashiria vya uvunjifu wa amani katika maeneo mbalimbali ili viweze kudhibiti mapema kabla hazijaweza kuleta athari.

 

"Tuwaache watu watimize majukumu yao ya kikatiba kwa amani na utulivu na Wala wasiogope kwenda kupiga kura kwani ulinzi umeimarishwa na kutakuwa na Hali ya usalama siku hiyo"alisema Chatanda


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments