DADA AMUUNGUZA KWA KISU CHA MOTO MAPAJANI , MASHAVUNI MDOGO WAKE AKIMTUHUMU KUCHEPUKA NA SHEMEJI YAKE


Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba (kulia), kushoto ni mfano wa kisu cha moto

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Jeshi la polisi mkoani Shinyanga linamshikilia Meckrida Masesa (25), mkazi wa Chela  wilayani Kahama kwa kosa la kumjeruhi mdogo wake mwenye umri wa miaka 15 (jina linahifadhiwa), mwanafunzi wa kidato cha pili shule ya Sekondari Baloha kwa kumuunguza sehemu za usoni, mashavuni na mapajani kwa kutumia kisu cha moto akimtuhumu kuchepuka na shemeji yake.


Kwa Mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba tukio hilo limetokea Septemba 28,2020 majira ya saa kumi na moja jioni katika kijiji na kata ya Chela, halmashauri ya Msalala wilaya ya Kahama.

Amesema mhanga alijeruhiwa kwa kuunguzwa na kisu cha moto na mtuhumiwa huyo ambaye ni dada yake wakiwa nyumbani kwa mtuhumiwa.

“Chanzo kikiwa ni wivu wa mapenzi baada ya dada yake huyo kumtuhumu  kuwa na mahusiano ya kimapenzi na shemeji yake ambaye ni mume wa mtuhumiwa huyo aitwaye Joseph Masolwa ambaye ni mwalimu wa shule ya msingi Chela”,ameeleza Kamanda Magiligimba.

 “Mtuhumiwa  alikiweka kisu hicho kwenye moto kwanza na kisha kuanza kumjeruhi mhanga. majeruhi anapatiwa matibabu katika kituo cha afya Lunguya na hali inaendelea vizuri”,amesema.

Kamanda Magiligimba anatoa wito wenzi/wanandoa kuacha kujichukulia sheria mkononi na badala wapeleke matatizo/migogoro yao ya ndoa kwenye ofisi za dawati la jinsia na watoto, viongozi wa dini,ofisi za ustawi wa jamii  ili kupata suluhisho la migogoro yao.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527