KATAMBI AENDELEA KUWASHA MOTO AKISAKA KURA SHINYANGA MJINI..AOMBA ACHAGULIWE ALETE MABADILIKO


Kulia ni Mgombea udiwani kata ya Ngokolo kupitia CCM Victor Mkwizu akimuombea kura mgombea ubunge jimbo la Shinyanga Patrobas Katambi katika mkutano wa kunadi sera uliofanyika mtaa wa Kalonga kata ya Ngokolo manispaa ya Shinyanga.

Na Suzy Luhende - Shinyanga 
Mgombea Ubunge Patrobas Katambi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) amewaomba wananchi wa jimbo la Shinyanga mjini wamchague ili aweze kuleta mabadiliko ya kimaendeleo katika jimbo hilo.

Hayo ameyasema jana wakati akinadi sera zake katika mkutano wa hadhara uliofanyika huko katika mtaa wa Kalonga kata ya Ngokolo manispaa ya Shinyanga ambapo amewaomba wananchi wamchague ili aweze kuleta mabadiliko ya kimaendeleo katika jimbo hilo.

Katambi amesema jimbo la Shinyanga lipo kama Kisiwa hivyo akichaguliwa atahakikisha anaboresha miundombinu ya barabara ili kuweza kuleta magari ya kubeba abiria, kama daladala za magari.

"Mkinichagua mji wa Shinyanga nitaubadilisha kutoka hivi ulivyo na kuwa na maendeleo zaidi na kuonekana mji wa kisasa zaidi, kama nilivyofanya mabadiliko katika mji wa Dodoma kwa mda mfupi nioaminiwa na mheshimiwa John Pombe Magufuli",amesema  Katambi.

Kwa upande wake mgombea udiwani kata ya Ngokolo kupitia CCM Victor Mkwizu amesema akichaguliwa atahakikisha anafanya mikutano mara kwa mara ili kujua kero zilizopo na kuweza kuzitatua kwa wakati. 

Amesema kata hiyo ilitakiwa kuwa na zahanati na kituo cha afya, hivyo wananchi wakimwamini na kumchagua atahakikisha anaanza kujenga zahanati ya kata ndani ya wiki mbili atakazoanza kazi.

Pia amesema wakati  wa mvua baadhi ya barabara waga hazipitiki hivyo akichaguliwa pia ataanza nazo ili kuweza kuondoa usumbufu kwa  wananchi wa kata hiyo.

"Naombeni mniamini ndugu zanguni mnichague ili niweze kuwatumikia kwa kuondoa zote zilizopo,  na tutaweka mitaro kila sehemu iliyo korofi nitaweka madaraja panapohitajika nitaweka makaravati pale panapohitajika na kuweka mitaro ya maji  ili inaponysha mvua maji yaweze kupitiliza",amesema

Amesema atakapochaguliwa kina mama wajasiriamali wanaouza mbogamboga na samaki watapata neema atakapochaguliwa kwani watakopeshwa ili kuongeza mitaji yao ikiwa ni pamoja na vijana watafaidika. 

Pia amesema ataboresha soko  mitumbani na soko la Majengo Mapya na kuwa masoko mazuri ya kisasa atajenga vyoo ili wafanyabiashara wasipate shida wanapotaka kujisaidia wakiwa kwenye biashara zao.
Kulia ni Mgombea udiwani kata ya Ngokolo kupitia CCM Victor Mkwizu akimuombea kura mgombea ubunge jimbo la Shinyanga Patrobas Katambi katika mkutano wa kunadi sera uliofanyika mtaa wa Kalonga kata ya Ngokolo manispaa ya Shinyanga. Picha na Suzy Luhende
Mgombea ubunge jimbo la Shinyanga Patrobas Katambi akiomba kura katika mkutano wa kampeni uliofanyika mtaa wa Kalonga kata ya Ngokolo manispaa ya Shinyanga.

Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia CCM, Patrobas Katambi akiomba kura kwa wananchi.
Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia CCM, Patrobas Katambi akimuomba kura Mgombea Udiwani kata ya Ngokolo kupitia CCM, Victor Mkwizu (kulia).
Mgombea udiwani kata ya Ngokolo manispaa ya Shinyanga Victor Mkwizu akiomba kura kwa wananchi wa mtaa wa Kalonga kata ya Ngokolo manispaa ya Shinyanga
Kashi Salula mdau wa maendeleo ambaye pia alikuwa mgombea ubunge jimbo la Shinyanga katika kura za maoni akimuombea kura Mgombea Urais kupitia CCM Dkt. John Pombe Magufuli, mbunge Patrobas Katambi, diwani Victor Mkwizu kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Ngokolo manispaa ya Shinyanga.
Kada wa CCM Godfley Malya akiomba kura za wagombea wa Chama Cha Mapinduzi akiwemo Dk. John Pombe Magufuli (Urais), Ubunge Parobas Katambi, udiwani Victor  Mkwizu kwenye mkutano wa hadhara wa kunadi sera uliofanyika mtaa wa Kalonga kata ya Ngokolo manispaa ya Shinyanga.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments