MAALIM SEIF AFUNGA RASMI KAMPENI ZA URAIS ZANZIBAR..

 Chama cha ACT -Wazalendo kimehitimisha kampeni zake za Urais visiwani Zanzibar, ambapo mgombea urais kupitia chama hicho, Maalim Seif Hamad, ametoa tathimini juu ya kampeni zake alizozifanya visiwani humo. 

Akizungumza jana  katika viwanja vya Mnazi Mmoja Visiwani humo Maalim amewahimiza Wazanzabari kujitokeza siku ya kupiga kura kwa ajili ya kuwachagua viongozi wanaowahitaji.

“Tumefanya kampeni na kwa tathimini yangu ni nzuri tuliwaeleza dhamira zetu,ahadi zetu na nini mtegemee kutoka kwetu ikiwa nitakuwa Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi”amesem Maalim Seif.

“Mambo mengi tumesema kubwa kuboresha maisha kuhakikisha kila Mzanzibari anapata ajira ,kuhakikisha vijana wetu wanapata elimu nzuri bila ya gharama mzazi”, Maalim Seif



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments