MGOMBEA WA UPINZANI ASHINDA UCHAGUZI WA URAIS USHELISHELI


Upinzani nchini Ushelisheli umeingia madarakani mara ya kwanza tangu mwaka 1977, baada ya kushinda uchaguzi wa urais.

Mchungaji wa Kianglikana Wavel Ramkalawan amemshinda Rais Danny Faure kwa 54.9% dhidi ya 43.5%, matokeo rasmi yanaonesha.

Wafuasi wa Bw. Ramkalawan wamekuwa wakisherehekea ushindi wake katika mji mkuu, Victoria.

Katika hotuba yake ya kihistoria, Mr Ramkalawan aliomba maridhiano kati yake na Bw Faure, akisema hakuna walioshindwa wala kushinda.

Taifa hilo lililokuwa koloni wa Uingereza lilipata uhuru mwaka 1976.

Chama cha Bw. Ramkalawan, United Party kiliingia madarakani kupitia mapinduzi mwaka mmoja baadae na kusalia madarakani baada ya demokrasia ya vyama vingi kurejeshwa mwaka 1993.

Katika tamko lake la kwanza baada ya kushinda, Bw. Ramkalawan alisema: "Mimi na Bw. Faure ni marafiki wazuri. Na kushindwa katika uchaguzi haimaanishi ndio mwisho wa mtu kuchangia ufanisi wa nchi yake.

"Katika uchaguzi huu, hakukua na walioshindwa, na hakuna walioshinda - nchi yetu imepata ushindi halisi."

Bw. Faure aliyekuwa amekaa karibu naye, alitikisa kichwa kama ishara ya kukubaliana na tamko la rais mteule, kulingana na ripoti ya shirika la habari la Reuters.


Kutaka mabadiliko

Uchambuzi wa mwanahabari Patrick Muirhead kutoka Ushelisheli

Matokeo ya uchaguzi huo yametikisa mazingira ya kisiasa katika taifa hilo la kisiwani.

Wafuasi wa Bw. Ramkalawan, mchungaji wanayemuita 'baba', wamemiminika katika barabara za mji mkuu, Victoria, wakipiga honi ya magari yao na kupeperusha bendera.


Ilikuwa mara ya saba kwa Bw. Ramkalawan kugombea urais katika uchaguzi.

Bw Faure, ambaye alirithi madaraka kutoka kwa mtangulizi wake miaka minne iliyopita alishindwa kutenga chama chake na tuhuma za mauaji ya kisiasa, ukatili na ufisadi wakati Ushelisheli ilipokuwa kwenye mfumo wa siasa wa chama kimoja.

Madaraka ambayo chama chake ilipata kupitia mapinduzi miaka 43 iliyopita yamechukuliwa kupitika kura ya wananchi waliokuwa wanataka mabadiliko.

Rais mpya anatarajiwa kuapishwa leo Jumatatu.

CHANZO- BBC SWAHILI


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments