NSSF YAENDELEA KUTOA HUDUMA KWA WANACHAMA NA WANANCHI KWA UJUMLA KATIKA MAONESHO YA CHAKULA NJOMBE | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, October 14, 2020

NSSF YAENDELEA KUTOA HUDUMA KWA WANACHAMA NA WANANCHI KWA UJUMLA KATIKA MAONESHO YA CHAKULA NJOMBE

  Malunde       Wednesday, October 14, 2020

Meneja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Njombe, Mrisho Mwisimba (kulia) akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa SIDO, Profesa Sylvester Mpanduji aliyetembelea banda la NSSF  katika maonesho ya Siku ya Chakula Duniani yanayoendelea mkoani Njombe. SIDO kwa kushirikiana na NSSF, Baraza la Taifa la Uwezeshaji Kiuchumi (NEEC), VETA na benki ya Azania kwa pamoja wanaratibu mpango wa kuendeleza viwanda vidogo na vya kati (SANVN VIWANDA SCHEME) ambapo tayari NSSF imeshatoa bilioni 5, huku SIDO na VETA wanahusika na utambuzi wa wajasiriamali, NEEC kazi yake ni kuratibu mpango huo na benki ya Azania inahusika kutoa mikopo hiyo.
Meneja wa NSSF Mkoa wa Njombe, Mrisho Mwisimba(kulia) akimpa maelezo Kaimu Katibu Mkuu wa Wiraza ya Kilimo, Dkt. Honest Kessy (Kushoto)alipotembelea maonesho ya Nane ya Siku ya Chakula Duniani yanayofanyika katika viwanja vya Mji Mwema mkoani Njombe.
Meneja wa NSSF Mkoa wa Njombe, Mrisho Mwisimba akizungumza katika maonesho ya Nane ya Siku ya Chakula Duniani yanayofanyika katika viwanja vya Mji Mwema mkoani Njombe, ambapo amewahimiza wananchi kujiunga na Shirika hilo ili wanufaike na mafao mbalimbali yanayotolewa na NSSF
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post