KATAMBI AJINADI KULETA NEEMA KWA WAFUGAJI, WAKULIMA, WAFANYABIASHARA


Na Marco Maduhu -Shinyanga. 

Mgombea ubunge wa jimbo la Shinyanga mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Patrobas Katambi, amemwaga sera zake kwa wananchi wa jimbo hilo, na kuahidi endapo wakimchangua kuwa mbunge wao atahakikisha anakuza uchumi wa wakulima na wafugaji.

Katambi amenadi sera zake leo kwenye mkutano wa kampeni eneo la Soko kuu la mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na wananchi, mgombea udiwani wa Kata ya Mjini Gulam Mukadam, wanachama wa chama hicho wakiwamo na viongozi, waliongozwa na mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa. 

Alisema kwa utafiti walioufanya Jimbo la Shinyanga mjini, halina wafugaji wa kutosha ambao wataweza kuhudumia kiwanda cha nyama pamoja na machinjio ya kisasa, na kuahidi wananchi endapo wakimchagua kuwa mbunge wao Oktoba 28 mwaka huu, atatenga eneo kubwa kwa ajili ya kufugia mifugo tu na kuinua uchumi wa mfugaji. 

“Mimi nataka kiwanda hiki cha nyama ambacho tutakifufua, pamoja na machinjio ya kisasa iliyopo, malighafi yake ambayo ni ng’ombe itoke kwa wazawa ambao ni wana-Shinyanga wenyewe ili muinuke kiuchumi,” alisema Katambi. 

Pia alisema kwa upande wa kilimo, ataleta taasisi ya utafiti ya kilimo (Tari), ili kubaini mbegu za kilimo ambazo zinakubalika maeneo ya Shinyanga, ili wananchi walime kilimo chenye tija ambacho kitawainua kiuchumi, na siyo kufanya kilimo cha kubahatisha. 

Katika hatua nyingine aliahidi kuboresha mazingira ya wafanyabiasha, ikiwamo kulikarabati Soko kuu la mjini Shinyanga, kuvutia wawekezaji, pamoja na wafanyabishara wa usafirishaji wakiwamo baiskeli za daladala, bodaboda, na bajaji, kuwapatia mikopo kupitia vikundi ili wapate kupanuka kibiashara. 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa, aliwataka wakazi wa jimbo la Shinyanga mjini siku ya kupiga kura Oktoba 28 mwaka huu wasifanye makosa bali wamchangue Katambi, pamoja na mgombea Urais John Magufuli, ili wawaletee maendeleo na Shinyanga iendane na uchumi wa kati.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini (CCM) Patrobas Katambi akinadi sera kwa wananchi.Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga ( Kulia) Mabala Mlolwa, akimnadi Mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini, Patrobas Katambi kwa wananchi ili wamchague awe mbunge wao Oktoba 28 mwaka huu.Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa, akiwataka wananchi wa Shinyanga wasifanye makosa kwenye uchaguzi mkuu Oktoba 28 mwaka huu, bali wamchague Katambi, pamoja na mgombea Urais John Magufuli ili wawa letee maendeleo.
Meneja kampeni wa mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini (CCM) Partobas Katambi, Gaspel Kileo akiwataka wananchi wa Shinyanga siku ya uchaguzi Oktoba 28 wakampigie kura Katambi pamoja na Mgombea Urais John Magufuli na madiwani wote wa CCM.Mfanyabiashara Gilitu Makula, akiwataka wananchi wa Shinyanga wampigie kura Katambi na Mgombea urais John Magufuli. Mgombea udiwani Kata ya Mjini Gulam Mkadamu akiwa amebeba mabango kwenye mkutano wa
Kampeni.
Wananchi wa Shinyanga wakiwa kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini CCM Patrobas Katambi.
Wananchi wa Shinyanga wakiwa kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini CCM Patrobas Katambi.
Wananchi wa Shinyanga wakiwa kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini CCM Patrobas Katambi.
Wananchi wa Shinyanga wakiwa kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini CCM Patrobas Katambi.
Wananchi wa Shinyanga wakiwa kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini CCM Patrobas Katambi.
Wananchi wa Shinyanga wakiwa kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini CCM Patrobas Katambi.

Na Marco Maduhu- Shinyanga.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments