Tanzia : MUIGIZAJI MAARUFU WA FILAMU YA JAMES BOND AFARIKI DUNIA

James Bond
Sir Sean Connery, muigizaji wa sinema ya James Bond amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 90, familia yake imethibitisha.

Muigizaji huyo wa Uskochi alifahamika sana kwa kuwa mhusika wa katika sinema ya James Bond, na alikuwa wa kwanza kuleta sinema hiyo katika ukumbi wa sinema.

Wasanii tofauti wameigiza nafasi ya James Bond katika filamu kadhaa, lakini mcheza sinema gwiji, Sean Connery, ndiye aliyecheza nafasi hiyo kwa mara ya kwanza.

Jason Connery, mtoto wa kiume wa nyota huyo aliyependwa na Waingereza wengi, amesema baba yake amefariki kwa amani akiwa usingizini mjini Nassau katika visiwa vya Bahamas, ambako ana nyumba yake, baada ya hali yake kutokuwa nzuri kwa muda mrefu.

"Wote tunafanyia kazi kuelewa tukio hili kubwa kwa kuwa ndio kwanza limetokea," aliongeza, akielezea kifo cha baba yake kuwa ni "pigo kwa watu wote duniani ambao walifurahia zawadi aliyokuwa nayo kama muigizaji.

Hafla ya heshima za mwisho kwa Connery itakayofanyika baadaye, kwa mujibu wa ofisa habari wake.

Kazi yake ya uigizaji wa miongo mitano ilimwezesha kushinda tuzo ya Oscar mwaka 1988 kutokana na jukumu lake katika 'The Untouchable'.

Filamu zingine alizoigiza Sir Sean ni pamoja na The Hunt for Red October, Highlander, Indiana Jones na the Last Crusade and The Rock.

Jason Connery alisema baba yake "alikuwa na sehemu kubwa ya familia yake Bahamas ambayo ilikuwa naye" alipofariki usiku mjini Nassau.

Alisema: "Sote tunajaribu kukubaliana na msiba huu mkubwa kwani limetokea sasa, ingawa baba yangu amekuwa mgonjwa kwa muda.

"Ni siku ya huzuni kwa watu wate waliomfahamu baba yetu mpendwa na watu wote waliovutiiwa na uigizaji wake kote duniani.

Sir Sean, anayetokea Fountainbridge, Edinburgh aliigiza filamu ya first James Bond mwaka 1962 na kuendelea mbele na kuigiza filamu zingine tano rasmi - na zingine ambayo sio rasmi kama vile Never Say Never Again mwaka 1983.

Aliamminiwa na watu wengi kuwa muigizaji mahiri ambaye aliigiza 007 kwa muda mrefu, akiitwa majina hayo.

Alikabidhiwa tuzo ya knigh na Malikia Queen katika Holyrood Palace mwaka 2000. Mwezi Augosti, alisherehekea mwaka wa 90 wa siku yake ya kuzaliwa.
Aliunga mkono kwa muda mrefu uhuru wa Uskochi, akisema hayo katika mahojiano kuelekea kura ya maoni ya mwaka 2014 na kugusia kwamba huenda akarejea nyumbani kutoka Bahamas na kuishi Scotland inadapo itapiga kura kujitenga na Uingereza.

Waziri wa Kwanza wa Scotland Nicola Sturgeon amesema: "Nimevunjika moyo kupokea taarifa za kifo cha Sir Sean Connery. taifa letu linaomboleza kwa kumpoteza mpendwa wetu.

Mcheza filamu huyo, ambaye pia alipewa na malkia wa Uingereza heshima ya kuwa Sir mwaka 2000, alitwaa tuzo kadhaa wakati wa kipindi cha uigizaji wake kilichodumu kwa miongo, zikiwemo tuzo za Oscar, Golden Globes na Bafta.

Lakini ilikuwa ni sinema maarufu ya 007, aliyoigiza akitumia Kiingereza chenye lafudhi ya Scotland akiigiza kama mpelelezi aliyekuwa na leseni ya kuua, iliyompatia umaarufu mkubwa duniani kote.

Alikuwa ni muigizaji wa kwanza kutoa maneno yasiyosahaulika ya "Bond, James Bond" na aliigiza filamu sita zilizotokana na mtunzi wa vitabu vya hadithi, Ian Fleming.

"Alikuwa na siku zote ataendelea kukumbukwa kama James Bond halisi," walisema watayarishaji filamu maarufu, Michael G. Wilson na Barbara Broccoli.

Mara kadhaa , mcheza sinema huyo kutoka Scotland alipigiwa kura na mashabiki ya kuwa muigizaji bora wa nafasi ya Bond, akiwashinda waigizaji wengine kama Daniel Craig wa sasa na Roger Moore.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments