SHIRIKA LA WORLD VISION LATOA VIFAA VYA ELIMU NA MICHEZO SHULE 14 SINGIDA


Afisa elimu mkoa wa Singida akikabidhi vifaa hivyo kwa niaba ya katibu tawala mkoa Nelas Mlungu moja ya walimu wailo fika kwenye makabidhiano ya vifaa kwenye ukumbi wa mkuu wa mkoa wa Singida.
Msaada wa vifaa zikiwemo runinga, taulo za kike, mipira na jezi kwa wasichana na wavulana.

Afisa Habari na Mawasiliano wa Shirika la World Vision Tanzania Agnes John azungumza na vijana balehe katika utekelezaji wa mradi huo.

Na Ismail Luhamba, Singida
Shirika World Vision Tanzania limetoa vifaa mbalimbali vya elimu na michezo ikiwemo taulo za kike vyenye thamani ya shilingi milioni 25, katika shule 14 za msingi na sekondari zinazotekeleza mradi afya ya uzazi kwa vijana balehe katika wilaya za Ikungi na Manyoni mkoni Singida.


Akikabidhi vifaa hivyo Mratibu wa shirika World Vision Mwivano Malimbwi alisema lengo la kutoa vifaa hivyo ni kuwasaidia vijana juu ya afya ya uzazi katika kupata elimu kupitia mradi wao wa afya ya uzazi kwa vijana balehe.

"World Vision kupitia wafadhili wetu tumetoa Televisheni katika shule za sekondari za Kintandaa,Dungunyi,Iglansoni,Salanda pamoja na Nkonko,na tumetoa vifaa vya michezo, taulo za kike katika shule za msingi na sekondari tulizoziteua katika hizo halmashauri", alisema Malimbwi.

"Tumetoa hizi taulo za kike kwa baadhi ya shule tulizoziteua kulingana na jiografia yake ya kuwa mbali na huduma mbalimbali za kijamii ili ziwasaidie vijana wa kike wanapoingia kwenye siku zao.nawaomba walimu wa hizo shule kuaandaa maeneo ya kutupa hizo taulo baada ya kutumika kwa lengo la kutunza mazingira",aliongeza

Malimbwi alieleza umuhumu wa kushughulikia afya ya jinsia na uzazi kwa vijana ambapo amesema vijana ni nguvu kazi na tegemeo katika uzalishaji mali,vijana ni raslimali,hivyo wanahitaji kuboresha afya zao ikiwa ni pamoja na afya ya uzazi ndio maana shirika hilo limekuja na program ya afya ya uzazi kwa vijana balehe katika mikoa ya Singida na Shinyanga.

Akipokea vifaa hivyo afisa elimu mkoa wa Singida kwa niaba ya katibu tawala mkoa Nelas Mlungu alilishukuru shirika kwa msaada wa vifaa hivyo kama Tv ambazo zitawasaidia wanafunzi hao kujifunza masuala ya afya ya uzazi.

Mlungu aliiomba jamii kusimamia malezi na maadili yaliyobora kwa vijana na wasisubiri mashirika na wadau wengine waje kusimamia masuala ya maadili.

"Tunawashukuru sana World Vision Tanzania kwa msaada wenu na nawaomba walimu mkasimamie vifaa hivyo visitumike vibaya bali vitumike kama ilivyotarajiwa", alisema Mlungu.


Hata hivyo walimu ambao shule zao zimepata msaada huo waliwapongeza World Vision kwa msaada wa vifaa hivyo kwani zitawasaidia watoto hao,na kwamba watahakikisha wanavitunza na kutumika ipasavyo.


Wanafunzi shule za msingi na Sekondari kutoka katika Wilaya ya Ikungi na Manyoni mkoani Singida, wakishiriki michezo ikiwa ni sehemu ya mradi wa afya ya uzazi na lishe kwa vijana balehe.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post