WATEJA WA TIGO SASA KUAMUA WENYEWE JUU YA UKOMO WA MUDA WA MATUMIZI WA VIFURUSHIMeneja wa kitengo cha bidhaa za intaneti, Ndevonaeli Eliakimu, akiongea na waandishi wa habari (Hawapo Pichani) wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ambayo inampa mteja uwezo wa kurefusha muda wa matumizi ya kifurushi ambacho kinakaribia kufikia ukomo wa muda wake wa matumizi. Kushoto kwake ni Meneja Mawasiliano wa Tigo Woinde Shisaeli Mapema leo Jijini Dar es salaam.


“Sasa ni muda wa kuchukua kilicho chako na Tigo, okoa bando lako kabla ya muda wake kuisha” Woinde Shisaeli-Meneja mawasiliano Tigo #TigoChukuaKilichoChako
“Tigo tunahakikisha tunakuwa wa kwanza kumpatia mteja bidhaa& huduma ambayo ataifurahia kila wakati, Sasa tumekuja na huduma ya kipekee ‘Chukua kilicho Chako’ ambapo mteja anaweza kuokoa bando lake kabla ya kuisha” Woinde Shisael-Meneja mawasiliano Tigo #TigoChukuaKilichoChako
·       Huduma hii ya kurefusha muda wa matumizi wa vifurushi ni ya kwanza na ya aina yake nchini Tanzania
Dar es Salaam. 8 Septemba 2020.  Kampuni inayoongoza kwa kutoa huduma bora za mawasiliano ya kidigitali nchini Tanzania, Tigo, leo hii imezindua huduma mpya ambayo inampa mteja uwezo wa kurefusha muda wa matumizi ya kifurushi ambacho kinakaribia kufikia ukomo wa muda wake wa matumizi. Huduma hii mpya itawapa wateja fursa na uwezo wa kuendelea kutumia kiasi cha kifurushi kilichobakia baada ya kufikia kikomo cha muda awali wa matumizi. Hii itahusisha vifurushi vya kupiga simu, kutuma meseji pamoja na data.
Huduma hii ya kuweza kurefusha muda wa matumizi kwa kifurushi kilichofikia kikomo cha muda wake wa matumizi maarufu kama ‘Chukua Kilicho Chako’ ni ya kwanza na ya aina yake na kampuni ya Tigo ndiyo ya kwanza inayompa uhakika mteja kuwa sasa hataweza kupoteza kifurushi chake ambacho hakijatumika.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hii mpya, Meneja wa kitengo cha bidhaa za intaneti, Ndevonaeli Eliakimu, amesema, “Kama mtandao wa kisasa wa mawasiliano nchini Tanzania, tumewasikiliza na tumeamua kufanyia kazi ombi hilo la wateja wetu ambao wamekuwa wakishindwa kutumia vifurushi vyao kutokana na kuisha kwa muda wake wa matumizi. Hivyo basi huduma hii mpya itawapa wateja uwezo wa kuongeza au kurefusha muda wa matumizi wa vifurushi vyao kuanzia siku, wiki hata mwezi”.
“Kama kampuni ya mawasiliano inayoongoza kwa kutoa huduma za kidigitali na za kisasa kabisa nchini Tanzania, tumekuwa wa kwanza kuzindua huduma hii mpya na ya aina yake hivyo wateja wetu sasa hawatakuwa na wasiwasi juu ya ukomo wa muda wa matumizi wa vifurushi vyao. Huduma hii inazidi kudhihirisha namna Tigo inavyojidhatiti kuhakikisha inawathamini wateja wake kwa kuwapatia huduma zenye ubunifu wa hali ya juu”, Eliakimu ameongeza.
“Hivyo basi kwa sasa vifurushi vitakuwa vinatumika kulingana na matakwa ya mteja na hii pia inadhihirisha ushindi kwa wateja wote wa Tigo nchini Tanzania na ni matumaini yetu kwamba huu ni mwendelezo wa kuboresha huduma zetu ili kumrahisishia mteja wetu namna ya kuwasiliana na wapendwa wake”, Eliakimu ameeleza.
Kupitia huduma hii, mteja atapokea ujumbe kila kifurushi chake kitakapokaribia kufikia mwisho wa muda wa matumizi, hivyo mteja ataweza kurefusha muda wa matumizi wa kiasi cha kifurushi ambacho kimebaki ili aweze kuendelea kukitumia mpaka kitakapokwisha.
                                           

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527