
Marehemu Turky amefariki katika Hospitali ya Tasakhta Global Kisiwani Unguja.
Swala ya kuombea mwili wa marehemu inatarajiwa kufanyika leo alasiri katika msikiti wa Othman Maalim na kufuatiwa na mazishi yatakayofanyika Fumba visiwani humo.
Marehemu Salim Turky alikuwa mfanyabiashara maarufu Zanzibar na mgombea ubunge wa Jimbo la Mpendae kwa tiketi ya CCM.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako