WEZI WAVUNJA MAHAKAMA,WAIBA SUKARI NJOMBE

Na Amiri Kilagalila,Njombe
Jeshi la polisi mkoani Njombe limewakamata vijana wawili kwa tuhuma za kuvunja Mahakama ya wilaya ya Njombe na kufanikiwa kuiba vitu mbali mbali ikiwemo sukari kilo 25,Kopyuta mpakato 3 na Mashine ya Pos inayotumiwa na mahakama.


Akizungumza na vyombo vya habari kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Hamis Issa amesema vijana hao ni pamoja ni Masood Mang’ombe na  Hamis Ismael ambao miongoni mwao amehusika na uvunjaji huku mwingine ni mnunuaji kutoka mkoa wa Ruvuma.

“Kuna watu wameenda wamevunja mahakama ya wilaya ya Njombe ikaibiwa vitu mbali mbali ikiwemo sukari kilo 25,Pos Mashine inayotumika na Mahakama na Laptop tatu,na washtakiwa wawili tumewakamata”alisema Kamanda Issa

“Sasa hivi tunangoja utaratibu ukamilike tuwafikishe mahakamani ili sheria ili ifuate mkondo wake.Yaani watu walivyokuwa majasiri hawaogopi hata vyombo vinavyowatendea haki kwenda kuwaibia”aliongeza Kamanda Issa

Vile vile kamanda Issa amesema wamefanikiwa kukamata mtandao wa watu wanaohusika wizi wa vifaa mbali mbali kwenye Magari zikiwemo taa,maturubai,Ekseli na Radio zinazoibiwa wakati magari yakiwa yamepaki mkoani humo.

“Vifaa hivi vinaibiwa kwenye magari,na leo hii tuna vifaa ambavyo tumewakamata navyo mtandao wa wezi.Tuna maturubai matano ya magari makubwa ambayo yanasafiri kutoka mikoa mingine,kuna vifaa vinaitwa Ekseli,halafu pia kuna Starter mbili za skania na kuna radi za gari ndogo kama kuna watu wameibiwa waje watambue”aliongeza Kamanda.

Kamanda wa polisi ametoa wito kwa wananchi kwenda kufanya kazi halali na kuto kujihusisha na mali za wizi ili kuepuka matatizo yanayoweza kujitokeza.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527