" MGOMBEA UBUNGE CHADEMA WANGING'OMBE AAHIDI KUINUA SEKTA YA KILIMO

MGOMBEA UBUNGE CHADEMA WANGING'OMBE AAHIDI KUINUA SEKTA YA KILIMO

Na Amiri Kilagalila,Njombe
Mgombea Ubunge jimbo la Wanging’ombe mkoni Njombe Dkt Dismas Luhwago (CHADEMA) amesema kama wananchi wakimpa ridhaa ya kuongoza jimbo hilo kwa miaka mitano atahakikisha sekta ya kilimo inakuwa na tija katika kukuza uchumi wa jimbo hilo kwa kuanzisha mikopo ya pembejeo na kusimamia kilimo cha mazao ya biashara yenye bei kubwa katika masoko ya kimataifa likiwemo zao la parachichi.Ameyasema hayo wakati akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Gonelamafuta kata ya kidugala ambapo amesema kuwa taarifa za kiutafiti zinaonyesha kuwa wilaya hiyo inafursa ya kuzalisha mazao ya biashara kama korosho,makademia na vanilla ambayo yana soko kubwa Katika masoko ya kimataifa na bado hayajaanza kuzalishwa.

“Tutaazisha mkakati wa kulima mazao ya biashara sio ya chakula,ya chakula mtalima kwa ajili ya chakula lakini tutakuwa na mazao ya biashara na parachichi namba moja” Alisema Luhwago

Amesema kuwa atasimamia serikali kuwasaidia wakulima kupata pembejeo za kilimo kwa haraka  kwa kupata mkopo kutoka bank ya kilimo.

“Serikali imeanzisha benki ya wakulima lakini kwa bahati mbaya wananchi wengi wa Wanging’ombe mlio wengi hamna sifa ya kukopesheka kwasababubu hamna sifa ya kukopesheka kwasababu hamna dhamana,mashamba yenu hayajapimwa,viwanja vyenu havijapimwa.Inamaana hamna hati tukishirikiana na serikali nitahakikisha tunapima maeneo yenu mpate hata hati za kimila,mimi nimewahi kopa hadi miioni ishirini kwa kutumia hati za kimila”aliongeza Luhwago


Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527