KONGWA YAANZA MKAKATI WA KILA KAYA KULIMA EKARI MOJA YA KOROSHO


Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Suleiman Serera akizungumza na Maafisa Ugani na Wakulima wakati akifungua mafunzo ya kilimo bora cha korosho yanayotolewa na Kituo cha Utafiti wa Kilimo TARI Naliendele Mtwara, wilayani humo mkoani Dodoma. Kushoto ni Afisa Kilimo Umwagiliaji na Ushirika wa Wilaya ya Kongwa, Jackson Shija na Mratibu wa Kitaifa wa Zao la Korosho kutoka  TARI Naliendele, Dkt.Geradina Mzena.

Mratibu wa Kitaifa wa Zao la Korosho kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo TARI Naliendele, Dkt.Geradina Mzena, akitoa mada kwenye mafunzo ya kilimo bora cha korosho yaliyotolewa kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa kwa Maafisa Ugani na Wakulima mkoani Dodoma. 

Mtafiti Mwandamizi na Mdhibiti wa Visumbufu vya wadudu na magonjwa kwenye zao la korosho, kutoka Tari- Naliendele  Dkt.Wilson Nene, akitoa mada kwenye mafunzo hayo.

Mtafiti  kutoka Tari- Naliendele Programu ya Zao la Korosho, Kasiga Ngiha, akitoa mada kuhusu 'Agronomia' ya korosho.

Meneja wa Bodi ya Korosho Kanda ya Kati na Magharibi, Ray Mtangi, akizungumzia masoko ya zao hilo.

Washiriki wakiwa katika mafunzo hayo.
Mafunzo yakiendelea.
Washiriki wakiwa katika mafunzo hayo.
Afisa Kilimo Umwagiliaji na Ushirika wa Wilaya ya Kongwa, Jackson Shija, akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Washiriki wakiwa katika mafunzo hayo.
Afisa Kilimo wa Kata ya Mkoka, Marcelin Chingilile, akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Mkulima wa Korosho wa Kata ya Mkoka, Rajab Singo, akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Afisa Kilimo wa Kata ya Mlali, Markusi Wongo, akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Mkulima wa Korosho, Sospeter Chiwuyo, akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Afisa Kilimo wa Kata ya Songambele, Asha Malekela, akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Afisa Kilimo wa Kata ya Zoissa, Emmanuel Mongi, akizungumza kwenye mafunzo hayo.


Godwin Myovela na Doto Mwaibale, Kongwa 

WILAYA ya Kongwa ipo mbioni kuanza kutekeleza mpango wa kuhakikisha kila kaya 
inalima ekari moja ya zao la miche ya mikorosho bora azma ikiwa ni kuongeza kipato sambamba na kusaidia kurejesha hali ya uoto wa asili na kupunguza athari za mabadiliko ya tabia nchi.

Hayo yalibainishwa jana na Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Suleiman Serera, wakati akifungua mafunzo ya Kilimo Bora cha Korosho yanayoendelea kutolewa na Kituo cha Utafiti wa Kilimo Tari Naliendele kwa wakulima na Maafisa Ugani wa Halmashauri wilayani hapa.

“Mkakati wa Wilaya ya Kongwa ni kuhakikisha angalau kila kaya inakuwa na ekari moja ya zao la korosho bora sababu ni zao la kudumu la kibiashara lenye manufaa kiuchumi, lakini tunataka kuikijanisha Kongwa yetu kupitia mbegu bora za mikorosho kutoka Tari Naliendele ,” alisema Serera.

Alisema ili kukamilisha mpango huo ambao hata hivyo tayari umeanza kutekelezwa kwa awamu itahitajika miche zaidi ya milioni 2 ili kuzifikia kaya zote 74,000 zilizopo ndani ya wilaya hiyo.

Serera alisema kilimo cha zao la Korosho katika Wilaya ya Kongwa kilianza rasmi msimu wa kilimo wa 2007l2008 na mpaka sasa kuna jumla ya mikorosho mikubwa 75,591 na midogo 231,295, hivyo kuwa na jumla ya mikorosho 306,886 sawa na ekari 10229.5.

“Naamini baada ya mafunzo haya maafisa ugani mtaendelea kutoa mafunzo ya kilimo bora cha korosho kwa wakulima kwenye maeneo yenu ili kuongeza tija na uzalishaji kwa ustawi wa wilaya yetu,” alisema Serera.

Kwa upande wake, Mratibu wa zao la Korosho Kitaifa kutoka Tari Naliendele, Dkt.Geradina Mzena alisema mafunzo hayo ya nadharia na vitendo yana lengo la kuongeza ujuzi kwa wakulima na maafisa ugani ili kuinua tija kwenye zao la korosho.

“Kwenye mafunzo haya pamoja na mambo mengine tutajikita katika kuangalia namna 
bora ya kuanzisha shamba jipya, ‘agronomia ya Korosho’ na namna bora ya kudhibiti wadudu na magonjwa ya zao hilo,” alisema Mzena. 
 

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments