KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA, AFCON LAPOTEA


Makamu wa Rais wa zamani wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Misri, EFA, Ahmed Shobir amesema kombe la AFCON limepotea katika makao makuu ya Shirikisho hilo.

Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON lilikuwa limehifadhiwa Misri baada ya timu ya Pharaohs kushinda kwa mara tatu mfululizo tangu mwaka 2006 hadi 2010.

Watendaji wa Shirikisho hilo wamedai ya kuwa kombe hilo lilikuwa limehifadhiwa kwa nahodha wa timu ya taifa, Ahmed Hassan. 

Hassan naye amekanusha hilo na kusema alikaa nalo kwa siku moja baada ya kushinda na alikambidhi tangu mwaka 2011.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527