KIKWETE: WAPINZANI WAMEISHIWA HOJA, CHAGUENI CCM IENDELEE KUWALETEA MAENDELEO | MALUNDE 1 BLOG

Thursday, September 10, 2020

KIKWETE: WAPINZANI WAMEISHIWA HOJA, CHAGUENI CCM IENDELEE KUWALETEA MAENDELEO

  Malunde       Thursday, September 10, 2020

Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Dk. Jakaya Kikwete, amekoleza moto kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM), huku akisema Watanzania wanapaswa kuendelea kukiamini chama hicho ili kushika dola.


Amesema CCM inastahili kupewa tena nafasi ya kuongoza ili kuwatumikia wananchi na kudumisha amani, upendo na kuwaletea maendeleo wanayoyahitaji.

Sambamba na hayo, Kikwete aliwaomba wananchi kutokubali kuyumbishwa na maneno ya wapinzani kwa kile alichodai wameishiwa hoja kwa kuwa yote wanayosema ni yale yaliyopita, ambayo CCM imeshayafanya muda mrefu.

Kikwete alitoa ahadi hiyo juzi wakati wa uzinduzi wa kampeni kwa nafasi za ubunge na udiwani mkoa wa Lindi, zilizofanyika katika uwanja wa Ilulu mjini hapa.

Alisema katika kipindi cha miaka mitano, mgombea urais wa CCM, Rais John Magufuli amefanya mambo mengi mazuri ya kimaendeleo, ikiwamo uboreshaji huduma za afya, elimu, nishati na utoaji mikopo kwa vijana na akina mama.

Katika kipindi hicho, alisema kwa mkoa wa Lindi pekee zimejengwa hospitali mbili za wilaya, vituo vya afya 16 na zahanati 70 zimeboreshwa katika halmashauri zote sita.

Licha ya uboreshaji wa huduma hizo, pia alisema mikopo 4,693 yenye thamani ya Sh. 2,313,534,500 imetolewa kwa vijana, kinamama, na watu wenye uhitaji maalum kupitia Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) na halmashauri za wilaya na manispaa.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post